MAKAMPUNI 112 KUTOKA NJE YA NCHI YATHIBITISHA KUSHIRIKI MAONYESHO YA 47 YA SABASABA


Na lilian Ekonga. Dar es salaaam

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini Tanzania (TANTRADE), imesema Takribani kampuni 112 kutoka nje nchi zimeweza kuthibitisha kushiriki kwenye Maonyesho ya 47 ya kimataifa ya Biashara (Saba Saba) ambayo yamepangwa kuanza Juni 28 mpaka Julai 13 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa leo May 19 na Bwn. Fortunatus Mhambe , Kaimu Mkurugenzi wa ukuzaji biashara wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania(Tantrade) wakati akizungumza na waandishi wa habar jijini Dar es salaam. 

Ambapo amesema lengo kuu la maonyesho hayo ni kuwakutanisha wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kwa kuchangamkia fusa mbalimbali zitakozopatikana katika maonesho hayo ili kukuza biashara zao kwa kuwapa fursa ya kutangaza bidhaa na huduam zao kwa lengo la kutafuta masoko katika nchi mbalimbali. 

 "Kauli Mbiu ya Maonyesho hayo nia TANZANIA MAHALA SAHIHI PABIASHARA NA UWEKEZAJI na maonyesho hayo yatakuwa na maendeo mbalimbali yalioboreshwa na program mbali mbali za kuvutia" amesema Mhambe

Ameongeza kuwa kwa mwaka huu tantrade waumeleta kionjo kipya ambapo kutakuwa na jukwaa muhimu la a wafanyabiashara kushiriki kunyeonyesha bidhaa zao na kutafuta masoko, eneo ambalo litatoa fursa kwa wafanyabiashra wa ndani na nje nchi kuonyesha bidhaa zoa.

"Katika jukwaa hili kutakuwa na waonyeshaji mbalimbali kutoka sekta ya Madini, sekta ya ujenzi, mazingira, sekta vijana , wanawake nanyingine nyingi" amesema  


Aidha ametoa wito kwa wafanya biashara kushiriki maonyesho hayo kupitia maeneo ikiwepo jukwaa la wafanyabishara kwa kunifunza kujenga uzoefu na ushirikiano.


 Pia Bw, Mhambe amesema nchi 14 zilizothibitisha kushiriki ni China, Umoja wa falme za kiarabu, uturuki , kenya , ghana , parkistani, Rwana, India, Singapor, indoneshia, siria , iran, Algeria, Parkistani na lengo leo likiwa ni kufikisha nchi 30 na wanaamini siku zilizobaki wanaweza kufikia hizo nchi 16 zilizobaki. 

"Tantarde imekuwa mdau mkubwa wa wafanyabiashara wadogo wadodo na kwa mwaka huu wametoa nafasi kubwa karibia sita kwa waonyeshaji ambao mwanzoni hatukuwa nao kwa kuonyesha huduma zao na bidhaa zao" amesema
Previous Post Next Post