KAMPUNI YA CILENT OCEAN YASIKIA KILIO CHA WAFANYABIASHARA WA TANZANIA WANAOTOA MIZIGO INDIA


Na Lilian Ekonga , Dar es salaam. 

Kampuni ya usafirishaji mizigo kwa njia ya maji imesikia kilio Cha Wafanyabiashara wa Tanzania wanaotoa mizigo Yao kutoka nchini India Kwa kufungua tawi katika nchi hiyo ambapo mizigo ama bidhaa za Wafanyabiashara hao zitaanza kusafirishwa moja Kwa moja kutoka Mumbai India kuja Tanzania. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi Hilo uliofanyika Leo Jijini dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni za silent ocean na Kilimanjaro star cargo Mohamed Soloka Amesema uwepo wa tawi Hilo nchini India hautamnufaisha tu mfanyabiashara pia utaiwezesha serikali kukusanya mapato yatokanayo na bidhaa zitakazo ingizwa nchini

"Mizigo yao mingi imekuwa ikikaa kwa muda mrefu kwenye kusafarisha kuanzia miezi mitatu mpaka miezi na sita sisi kama silent ocean tuliona hii changamoto na kutakaamua kufungua tawi kwaajili ya kusaidia wafanyabiashara" amsema soloka



Ameongeza kuwa Mizigo yao mingi imekuwa ikikaa kwa muda mrefu kwenye kusafarisha kuanzia miezi mitatu mpaka miezi sita na wao kama sisi kama silent ocean waliona hii changamoto na kuamua kufungua Tawi ili kuweza kuwasaidia wafanyabiashara.

Kwa upande wao Wafanyabiashara kutoka soko la kariakoo waliohudhuria uzinduzi huo wameeleza kwamba fursa hiyo itawawezesha Wafanyabiashara wa Tanzania kusafirisha bidhaa zao Kwa muda mfupi yaani siku 17 hadi 25 ambapo hapo awali bidhaa zilikuwa zikisafirishwa Kwa muda wa miezi mitatu hadi sita.

Sisi wafanyabiashara tumepitia changamoto nyingi sana za usafirishaji wa bidhaa kwa muda mrefu sana kwa kipindi kirefu tumekuwa tukisafirisha bidhaa kwa muda mrefu sana kwanzia tunapo nunua India mapaka kutufikia sisi Dar es salaam, 

Aidha wameipongeza serikali Kwa kuamua kutatua changamoto za Wafanyabiashara wa soko la kariakoo na wanaamini kwamba kukutana na Waziri mkuu Kwa siku ya kesho kutawapa mwanga Wafanyabiashara juu ya changamoto ya Sheria ya maghala ambayo wanadai kuwa haiwatendei haki
Previous Post Next Post