KAMATI YA BUNGE YA UWEKEZAJI ( PIC ) YATEMBELEA MIRADI MIKUBWA MITATU YA NHC


Na lilian Ekonga, Dar es salaam

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), imefanya ziara ya kutembelea Miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mradi wa Morocco Square, Mradi 7/11 uliopo kawe pamoja na Mradi wa Samia Housing Scheme uliopo tanganyika Packers Kawe Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) Mhe. Jerry Silaa baada ya kumaliza kutembelea miradi hiyo amesema Mashirika ya umma yameudwa kufanya kazi ya kutengeneza faida kwa kuhakikisha wanafanya mipango ili kufikia malengo waliojiwekea kama miradi ya Morroco square na 7/11 ambayo imegarimu Taifa.


"Shirika la nyumba NHc ni shirika mkombozi kwa makazi ya mtanzania kwakuwa wamekuwa wakirahisha kwenye ujenzi wa nyumba ambapo unanua nyumba ambayo imeshajengwa tayari na kuoka mda wa kusimamia ujenzi" amesema Jerry.

Pamoja na hayo kamati ya Bunge imetoa wito kwa mashirika ya kibiashara ya umma kuhakikisha wanashirikisha serikali katika mipango yao ili kuweza kufahamu garama za kusimamisha miradi mikubwa kwa lengo la kuwafahamisha watanzania. 


Pia kamati hiyo imempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuifufua miradi hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Nyumba la Taifa ( NHC) Bw. Hamad Abdallah, Ameishukuru kamati ya bunge ya kwakutenga muda wao na kuthamini majukumu ambayo wamepewa na taifa hili ya kusimamia mashirika ambayo yanafanya uwekezaji.

Ameongeza kuwa mradi wa morocco square umekamilika kwa asilimia 97 na mda si mrefu wataruhusu wapangaji na Mradi wa Samia Housing Scheme unaendelea na ujenzi na wanatarijia kumaliza mwisho wa mwaka huu mwenye nyumba takribani 560 na wanunuzi wameshapata kwa asilimia 80.


"Mradi wa 7/11 ambao ulikuwa umesimama tangia mwaka 2017 na serikali ya awamu ya sita umeweza kuikwamua hiro miradi na kufikia mwezi wa saba mkandarasi atakuwa amerudi kazini na kuendela na ujenzi ni mradi wa nyumba 422 za makazi maeneo kwaajili ya biashara na michezo" amesema Abdallah

Aidha amemuhakikishia Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma PIC kusimamia miradi hiyo kwa garama sahihi ikiwemo vifaa kuchukua moja kwa mona kutoka viwandani.
Previous Post Next Post