MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AMEZITAKA MAMLAKA ZOTE ZA MAJI KULIPA MADENI IFIKAPO ROBO YA MWAKA 2023


Na Lilian Ekonga Dar es salaam

Makamu wa Rais Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango amezita mamlaka zote za Maji nchini ambazo zinakabiliwa madeni na kuchangia kuzorotesha utoaji wa huduma za maji kuhakikisha wanalipa malimbikizo ya madeni hayo ifikapo robo ya mwaka 2023.

Ameyasema hayo Leo katika hafla Uzinduzi wa Taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za Maji safi na Usafi wa Mazingira kwa mwaka 2021/22 iliandaliwa na Mamlaka ya uthibiti wa Huduma za nishati na Maji (EWURA) iliyofanyika Jijini Dar es salaam.

Sambasamba na hilo Makamu wa Rais amekabidhi vyeti kwa mamala za maji 38 kati ya 90 zilizofanya vizuri kwa mwaka 2021/22

Pia amezitaka mamlaka za Maji kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuzoea wateje kwani wananchi wamekuwa wakitoa malalamiko mbalimbali ikiwemo kutoa kuapta huduama kwa wakati.

"Wamekuwepo watumishi mamlaka za maji ambao sio waajiliwa na watu wanachafua sana jina la wizira na mamalka za maji kwa kuwakoswa wananchi
Namuwagiza Naibu waziri wa Maji kuhakikisha wanadhibiti vishoka na mtumushi yoyote atakaye shirikiana nao haondolewe" amesema Dkt Mpango

Aidha ameitaka EWURA kuhakikisha wanaongeza nguvu kwa kukagua ankara za maji zinazotolewa kwa wananchi kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama na kuboresha huduma kwa ya utoaji maji.

Kwaupande wake Naibu katibu wa wizara maji Eng Cyprian Luhemeja amesema kwa dunia watu bilion 2 wanakabiliwa na changamoto maji safi na salama ambapo kwa tanzania nchi imewezeka na kupiga hatua zaidi vijiji elfu Tisa vinapata huduma ya maji na salama ikiwa ni sawa na asilimia 77.

Nea Mkurugenzi wa Mamalaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA )Dkt James Andilile , amesema wametoa taarifa 14 tangi kuanzishwa kwa Mamalaka na lengo ni kufanya tasmini ya mamalka za maji na kutatua changamoto katika huduma za maji na usafi wa mazingira na kuangalia vipaumbele katika wizara maji na usafi wa Mazingira.

"Ewura itaendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha mamlaka za maji zinakuwa na huduma bora kwa kuwezesha na kuandaa mipango na kuwa na mikataba kwa huduma kwa wateja na kutoa miongozi mbalimbali katika huduma za maji" amesema Dkt Andilile.
Previous Post Next Post