SOAH: SHERIA YA HABARI YA MWAKA 2016 ILINYIMA UHURU WA KUJIELEZEA


Na Humphrey Msechu

Mkuu wa chuo cha uandishi wa habari Dar es salaam (DSJ ) ambae pia ni mwanahabari na mdau wa masuala ya habari, Bw. Johnson Soah amesema mabadiliko ya sheria ya huduma za za habari ya mwaka 2016 yana tija kwasababu baadhi ya vipengele vya sheria hiyo viliminya uhuru wa kujieleza , habari na wanahabari wenyewe.

Soah ameyasema hayo wakati wa mahojiano maalum na Sparklight Media kuhusu mchakato wa mabadiliko ya sheria ya huduma ya vyombo vya habari ambayo muswada wake ulisomwa Bungeni kwa mara ya kwanza mwaka huu kupitia mabadiliko ya sheria ndogo ndogo.

" Kufanyiwa mabadiliko kwa sheria hii kutaleta mabadiliko katika uhuru wa kujieleza na wanahabari watafanya kazi zao kwa uhuru bila kuminywa kwa uhuru wa kujieleza " amesema 

Kuhusu upande wa ufundishaji Soah amesema kuwa mbadiliko yataleta tija kwasababu wakufunzi wa uandishi wa habari wanafundisha sheria kwa kutumia sheria iliyopo sasa ambayo wadau wa habari wanaipigia kelele na kutaka ibadilishwe hivyo ikibadilishwa hata namna ya ufundishajaji itabadilika pia kulingana na madaliko hayo.

Amesema waandishi wa habari wa baadae wataitumia sheria hiyo vizuri katika kuandaa, kutafiti , kutafuta na kuandika habari ikiwemo habari za uchunguzi bila kizuizi chochote .
Previous Post Next Post