HAKIELIMU YATOA WITO KWA SERIKALI KUCHUKUA HATUA KALI DHIDI YA WOTE WATAKAO BAINIKA KUFANYA VITENDO VYA UKATILI KWA WATOTO


Na Mwandishi Wetu

Kufuatia video iliyokuwa inasambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha Mwalimu akimuadhibu mwanafunzi sehemu za nyayo za miguu kinyume na taratibu Shirika la HakiElimu limetoa wito kwa Serikali kuchua hatua ambazo zitakomesha kabisa matumizi ya viboko kwa watoto shuleni na kuhimiza adhabu chanya/mbadala ambazo sio za kikatili na zinazozingatia misingi ya haki za Binadamu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Januari 26 Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu , Dkt. John Kalage amesema kuwa shirika hilo limepokea kwa masikitiko tukio hilo na kusisitiza kuwa kitendo hicho sio tu kinakiuka haki za watoto bali pia ni kinyume na maadili ya kazi ya ualimu na malezi bora ya wanafunzi.

Kalage amesema wanaipongeza Serikali kupitia Waziri wa Elimu Pro. Adolf Mkenda na uongozi wa mkoa wa Kagera kwa kuchukua hatua za haraka ikiwemo kumsimamisha kazi mwalimu aliyefanya kitendo cha ukatili kwaajili ya kupisha uchunguzi.

"Tunaipongeza serikali kupitia wizara ya Elimu , Sayansi na teknolojia Mhe. Adolf Mkendana uongozi wa mkoa wa Kagera kwa kuchukua hatua za haraka na za awali dhidi ya mwalimu aliyehusika na Ukatili huo ikiwa ni pamoja na kumvua nafasi yake ya Ualimu Mkuu, kumsimamisha kazi na kuunda tume ya kuchunguza tukio hilo ili hatua za kisheria ziweze kufuata" amesema Kalage.

Ameongeza kuwa kuna haja ya serikali kuweka mipango endelevu ya kuimarisha mifumo rasmi ya ulinzi na usalama wa watoto shuleni ikiwa ni pamoja na kuharakisha uanzishwaji wa madawati ya ulinzi na usalama wa mtoto shuleni pamoja na mabaraza ya watoto .

Amesema serikali ichukue hatua kali dhidi ya wote watakaobainika kuhusika na kitendo vya ukatili dhidi ya watoto ili kukomesha vitendo hivyo ndani na nje ya shule.
Previous Post Next Post