WAZIRI NAPE: MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI KUFANYIKA JANUARI 2023


Na Humphrey Msechu

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewahikikishia wadau wa sekta ya habari kuwa marekebisho ya sheria ya huduma za habari yanakwenda kufanyika Januari 2023.

Amesema mabadiliko hayo ni safari ya kuwezesha kulindwa kwa uhuru wa habari kwa mujibu wa sheria na sio utashi wa viongozi.

Nape ameeleza kuwa wakati hilo likisubiriwa, uhusiano baina ya sekta ya habari na sekta ya umma umeendelea kuimarika katika awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.


Nape ameyasema hayo leo Desema 17, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongamano la kwanza la maendeleo ya sekta ya habari lililoandaliwa na wizara hiyo na kuwakutanisha wadau zaidi ya 1000 wa sekta hiyo.

“Sheria na kanuni mbalimbali zinaendelea kufanyiwa mabadiliko kwa mujibu wa sheria. Uhuru wa habari unapswa kulindwa kwa mujibu wa sheria sio utashi wa viongozi. Kiongozi yeyote atakayekuja atalazimika kuulinda uhuru huu kwa mujibu wa sheria hata kama hataki" amesema



Previous Post Next Post