WALIMU WAASWA KUTOKUTUMIA VIBOKO KWA KUDHANI WANAFUNZI WATAPENDA KUSOMA NA KUFAULU VIZURI


Na Lilian Ekonga.

Kamishna wa elimu Tanzania Dkt. Lyabwene Mtahabwa, ameto rai kwa walimu kuachana na kitendo cha kutumia viboko kwa kudhani kwamba wanafunzi watapenda kusoma na kufaulu ambapo si mtazamo sahihi. 

Ametoa Rai hiyo leo Disemaba 16 katika Kikao cha Kujadili maendeleo mradi wa Maendeleo ya Elimu ya Ualimu( TESP), unaodhaminiwa na serikali ya Canada jijini Dar es salaam ambapo amewasihi walimu kuachana na vitisho katika ngazi mbalimbali za elimu ya Awali mpaka vyuo vikuu kwani vinaua elimu ya Tanzania.

Amesema Mradi huo unalenga kuwabadilisha walimu kuona ni kazi ya samani inayopaswa kufanywa kwa uangalifu mkubwaa maana mwalimu anaweza kuua taifa ama kuponya taifa.


"Tutaangalia nini kimefanyika ndani ya mradi huu ulianza 2017 na kuisha 2025 ili kuweka mikakati ya namna ya kuendeleza mradi huu kwa yale mazuri yasikome tanzania bali yaendelee"amesema Dkt Mtahabwa. 

Kwa upande wake katibu wa Mradi wa TESP Cosmas Mahenge, amesema mradi huo umejikita katika kuimrisha Elimu ya Ualimu nchinj hasa katika ngazi ya Astashahada na Stashahada katika vyuo vya Ualimu nya serikali.

"Kazi zilizofanyika na mradi ni kutoa mafunzo katika vyuo vya ualimu kwa wakufunzi takribani 1300 na wote wameweza kupatiwa mafunzo mbalimbali ikiwemo tehema,mafunzo ya kijinsia, mafunzo ya masomo ya kufundishia pamoja na mafunzo ya kitaalamu ya ualimu zaidi"amesema Mahenge

Pia amesema mradi huo umewekeza katika utoaji wa vifaa vtehema katika vyuo vyote 35 kama kompyut, projector na vingine mbalimbali.

Ameongeza kuwa mradi huo umeweza kurabati vyuo saba na cha nane ni chuo cha ualimu kilichopo korogwe ambapo umeweza kukarabati maktaba kubwa ambayo ilikuwa haijaisha kwa mda mrefu.

Aidha amesema mradi wa TESP umesaidia kujenga maktaba mpya kubwa za kisasa na kukarabati maabara za tehema pamoja na maabara za sayansi na mradi umewekeza katika kuimarisha uongozi katika vyuo vya ualimu na kupatia mafunzo kwa viongozi wa taasisi za Elimu.

Nae Mwenyekiti wa vyuo vya serikali Tanzania bara Agustino sahili, emesema wamenufaika na mradi huo kwa kupata mafunzo kwa wakufunzi wote.

Ameongeza kuwa wamepata manufaa ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu kwa vyuo vinavyojihusisha na maswala ya sayansi kujengewa maktaba mpya, na vyuo vingine vimepata ukarabati mbalimbali.
Previous Post Next Post