Kiwanda cha magari cha GF Vehicles Assemblers (GFA) cha shinda tuzo ya Ubora 2022\2023 kwa makampuni makubwa nchini


Na mwandishi wetu

Kiwanda cha kwanza cha kutengeneza na kuunganisha magari nchini Tanzania GF cha Vehicles Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwan kimeibuka mshindi wa kwanza kwa makampuni makubwa nchini wakati wa utoaji wa tuzo  za  Ubora wa Kitaifa wa makampuni bora kwa  Mwaka 2022\2023  zilizoandaliwa na shirika la viwango nchini TBS.


Akizungumza wakati wa hafla hiyo Kiwanda cha hicho, Ezra Mereng alisema  wanaipokea tuzo hiyop kwa furaha kutokana na kushiriki kwa mara ya kwanza na kuibuka kuwa washindi wa jumla katika kipengele cha makampuni makubwa.

Pia alisema tuzo hiyo inawahamasisha kuendelea kufanya kazi kwa bidi Zaidi ikiwezekana mwakani washinde tuzo za kimataifa za ubora wa bidhaa na itakayoweza kuzalisha magari na kuingia katika soko la ushindani kimataifa.Pia aliwashukuru wafanyakazi wenzake wakiongozwa na timu mzima ya wataalamu katika kutengeneza magari vitengo tofauti.


Nae mkurugenzi wa shirika la viwango nchini (TBS) ..aliwataka  GF kutoridhika na ushindi huo wa jumla nchini na wahakikishe wanashiriki mashindano  ya  nchi ya SADC katika ubora na viwango kwa makampuni ya jumuia hiyo kuibukja mshindi anapata tiketi ya moja kwa moja ya kushiriki  mashindano ya Uboroa na viwango ya  jumuia ya SADC  na atakuwa anaiwakilisha Tanzania  na wao kama TBS watashirikiana na GF kuhakikisha wanapeperusha vyema benderaya Tanzania.

Kwa kumalizia mkurugenzi Mtendaji wa  GF Vehicles Assemblers (GFA) Imrani Karmal   anawapongeza  wafanyakazi wake kwa umoja wao ndio chachu ya mafanikio ya wao kukidhi Ubora  katika uzalishaji wa magari bila wao wasingweweza kufanikiwa katika ushindi huo.
Previous Post Next Post