KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA AFUNGA OFISI DAR ILI VIONGOZI WATII AGIZO LA KUHAMIA DODOMA


Na. WAF-  Dar es Salaam,

Menejimenti ya Wizara ya Afya chini ya Katibu Mkuu Prof. Abel Makubi imechukua hatua za kuifunga Ofisi ya Uratibu wa Miradi wa Ukimwi, TB na Malaria (COAg) iliyopo chini ya Wizara ya Afya ambayo inasimamiwa na Dr Peter Mgosha kwa kukaidi agizo la Rais na Waziri Mkuu kuhamia makao makuu  Dodoma.


Prof. Makubi amebainisha hayo Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Dkt. Mgosha amekaidi zaidi ya mara tatu agizo la kuhamia Dodoma pamoja na kukumbushwa na Menejimenti ya Wizara. 

Katibu Mkuu ameagiza watumishi wote wa ofisi hiyo wafike Dodoma Jumatatu bila kukosa.


Menejimenti imechukua hatua ya kufunga ofisi hiyo na hatua zingine  za kinidhamu ziendelee chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu.
Previous Post Next Post