DKT. MPANGO AIPONGEZA TAASISI YA MECIRA KWA KUFICHUA UHARIBIFU WA MAZINGIRA UNAOFANYWA KWENYE MAENEO YENYE VYANZO VYA MAJI


Na Mwandishi Wetu, Iringa

Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango ameipongeza Taasisi ya Mecira kwa kufichua uharibifu wa Mazingira unaofanywa kwenye pori tengefu la loriondo, bonde na Ihefu na maeneo mengine yenye vyanzo vya maji.

Amesema hayo leo tarehe 19, Desemba 2022 wakati akifungua rasmi Kongamano la Wahariri na Wadau wa Uhifadhi, Mazingira na utunzaji vyanzo vya maji linalofanyika kwenye ukumbi wa Masiti Iringa.

"Napenda kuipongeza taasisi ya Mecira kwa kufichua maeneo yenye uharibifu wa mazingira ikiwemo pori tengefu la Loliondo, hifadhi ya Ngorongoro,bonde la Ihefu likivamiwa na maeneo ya vyanzo vya maji, serikali na mimi binafsi tunawapongeza " alisema Dkt.Mpango

Pia Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango amezikumbusha Wizara zote, Mikoa yote pamoja na Taasisi za Serikali kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa katika utunzaji mazingira.

"Ili kulilinda bonde la Ihefu, nazikumbusha wizara zote zinazohusika, mikoa yote, taasisi zote pamoja mabonde, kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na serikali ikiwemo kuweka alama za mipaka" Alisema Dkt. Mpango

Sanjari na hayo Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango amewaagiza viongozi wa mabonde nchini kuchukua hatua kwa wahusika ikiwemo kubomoa miundombinu iliyojengwa kuzuia mito bila vibali huku akiwaagiza viongozi wa mamlaka za maji kuwasilisha ofisini kwake vibali kwa waliopewa
 
Previous Post Next Post