WANAWAKE WAJAWAZITO ZAIDI 200 WAKABIDIWA VIFAA VYA KUJIFUNGULIA KATIKA HOSPITALI YA MBAGALA ZAKHIEM


Na Mwandishi wetu, Dar es salaam

Wanawake wajawazito na walio katika uzazi baada ya kujifungua wameshauriwa kuzingatia mazoezi pamoja na lishe bora ili kuepuka vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na lishe duni na kutozingatia mazoezi.

Ushauri huo umetolewa jijini Dar es Salaam na mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya  Temeke Theodora katika zoezi la ugawaji vifaa vya kujifungulia kwa zaidi ya wanawake 200 wajawazito katika hospitali ya Mbagala Zakhiem.


Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Hatua Africa kupitia mradi wake wa Busela Derick Mgaya amesema ukosefu wa elimu ya afya ya afya kuhusu lishe bora na mazoezi kwa mama wajawazito ni chanzo cha vifo vya mama na mtoto.

Hata hivyo baadhi ya mama wajawazito wamesema iwapo elimu ya afya na mama na mtoto itaendelea kutolewa na taasisi mbalimbali  itaokoa maisha ya mama wajawazito na watoto hasa walio katika mazingira duni.

Aidha Mkurugenzi wa taasisi ya Hatua Afrika amesema utoaji elimu ya afya kwa mama wajawazito juu ya masuala ya lishe na mazoezi kwa mama wajawazito hadi mwaka 2024 unalenga kuwafikia zaidi ya wanawake laki tatu nchi nzima lengo kupunguza vifo vya mama wajawazito.

Previous Post Next Post