WAZIRI NAPE, MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA POSTA DUNIANI


Na mwandishi wetu

Shirika la posta Tanzania limeandaa maadhimisho ya wiki ya posta Duniani yatakayoanza tarehe 8 Octoba na kumalizika tarehe 9 Octoba 2022 ambapo mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Waziri wa habari mawasiliano na teknolojia ya habari Nape nnauye.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Elia Madulesi, amesema katika maadhimisho shirika la posta litakuwa na uzinduzi wa huduma mbalimbali na mijadala mbalimbali inayohusu biashara mtandao na anuani za makazi.

"Tarehe nane tutakuwa na kongamano kubwa JNICC litakalokuwa na mijadala inayohusu biashara mtandao na anuani za makazi hivyo watabadilishana wataalamu wa mitandao shughuli za posta na namna ambavyo anuani za makazi zinatumika"Amesema Madulesi.

Amsema Siku hiyo kutakuwa na wataoa mada mbalimbali na mada mbalimbali zitajadiliwa n  wanatarajia kwwafanyabishara na wajasiriamali watashiriki kwa wingi kwenye maadhimisho Hayo.

Pia Madulesi amesema kutakuwa na warsha ya watoa huduma wa mawasiliano wa mambo ya posta  itakayofanyika TCRA Oktoba 7 mwaka huu ambapo wataongea mambo mbalimbali ikiwemo utoaji wa huduma, kanuni, ubora na mambo ya kuzingatia katika utoaji wa huduma na uboreshaji wake


Aidha  kufuatia kuwepo kwa tukio la kusaini makubaliano ya kufanya biashara na posta ya Oman,  Madulesi amesema tayari matunda yameanza kuonekana na wahusika wa Oman watakuwepo siku hiyo ya maadhimisho,  ambapo kutakuwa na uzinduzi wa Stemp maalum ambayo imechapishwa kwa ushirikiano wa posta ya Tanzania na Oman.

Mbali na hayo,Madulesi amesema kulikuwa na mashindano kwenye mafungu matano, hivyo katika maadhimisho hayo itakuwa ni siku rasmi ya kuwatangaza na kuwapa zawadi wale washindi waliofanikiwa kushiriki na kushinda kwenye mashindano hayo.

Kwa upande wake Meneja Barua na Usafirishaji kutoka Shirika la Posta Tanzania, Jason Kalile amesema baada ya kugundua kuwa kuna gepu kubwa lililopo kati ya mawasiliano ya aina fulani ya jamii na kundi kubwa la watu wenye umri mkubwa kwenye simu na mitandao ya kijamii, kifedha na vitu shirika likaja na mkakati wa kumuwezesha mwananchi kwa namna ya kipekee.

"Tumeangalia gepu kubwa la uagizaji wa vitu kutoka sehemu moja kwenda sehemu ingine ndiyo maana tunaanzisha duka mtandao na posta kiganjani hivyo pale ambapo umeagiza huhitaji tena kutumia karatasi na kalamu bali utatumia simu yako"

Kaulimbiu ya mwaka huu katika maadhimisho hayo ya Octoba tisa ya wiki ya posta Duniani ni 'Posta kwa kila mtu'
Previous Post Next Post