WAZIRI NAPE AMEZINDUA STAMPU YA PAMOJA YENYE HISTORY YA NCHI TANZANIA NA OMAN


Na Judith Chao, Dar es salaam

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye leo  katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani tarehe 9 oktoba 2022, Amezindua Stampu ya Pamoja yenye historia ya Tanzania na nchi ya Oman,Yenye Kauli Mbiu ya POSTA KWA KILA MTU.

Akizungumza wakati Uzinduzi Huo uliofanyillka Leo jijin dar es Salaam Waziri Nape amesema Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Samia Imejipanga kuwawazesha watoa Huduma za posta kuwafikia wananchi Kwa urasi bila kufika Katika ofisi za posta.


Pia Waziri Nape amezindua mfumo mpya wa Posta Kiganjani ambao utabeba Huduma zote za shirika la posta na kuziweka mahali pamoja ndani ya simu ya kiganjani 

Katika uzinduzi uwo amesema hili litawezekana kwakuwa Serikali imeshakamilisha utekelezaji wa mfumo wa Anuani za Makazi ambao ni miundombinu Muhimu Katika utoaji wa Huduma" amesema Waziri Nape.

Waziri Nape amesema historia ya Oman na Tanzania ni ndefu na imezunguka sana ni Muhimu historia hii kulindwa na wao shirika la posta wameamua kuongoza kulinda historia hiyo.


Pia waziri amewapongeza viongozi wa shirika la posta wa Tanzania na Oman Katika kushirikiana na kuzindua stempu ya Pamoja.

Waziri Nape  ametoa wito Kwa shirika la Posta kuongeza Nguvu Kwenye  kubuni biashara nyingine za kiposta zinazoenda na matuzi ya Technolojia Ili kukidhii mahitaji mapya ya wateja.

Sambamba na hilo  Waziri Nape amekabidhi zawadi kwa vilele wa kushindania mashindano  mbalimbali ,Kama uwandishi wa Makala,wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Posta.

Waziri Nape  amewasihi wa Watanzania kutumia Huduma za posta ambazo zimeboreshwa kwakuwa posta ya Sasa si barua tuh ni Zaid ya barua"
Previous Post Next Post