KAMPUNI YA MAGARE YAJIVUNIA UBORA WA BIDHAA ZAKE


Na Humphrey Msechu, Geita

MENEJA wa Uendeshaji wa Kampuni ya Magare, Allan Kisoi Ametoa wito kwa watanzania tembelea kwenye Maonyesho ya tano ya kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika mkoani Geita ili kujionea aina za bidhaa ambazo wanazalisha kupitia kiwanda chao.

Amesema kuwa kupitia maonyesho hayo ya madini wao kama kampuni ya Magare wamekuja na bidhaa mbalimbali zikiwemo vifaa vya maalumu vya sehemu ya kazi migodini (PPE) Nguo za aina mbalimbali, Mashati ya ofisini ,suluali aina ya Kadeti,nguo za ndani,(BOXER) viatu vya shule kwa ajili ya watoto kuazia darasa la kwanza hadi kidato cha sita.


Allan ameyasema hayo leo oktoba 2 mwaka huu katika mahojiano maalumu yaliyofanyika kwenye viwanja vya maonyesho ya Madini Bombambili mkoani humo.ambapo pia amesema kuwa licha ya bidhaa hizo lakini pia kuna mikanda ya kiunoni,viatu vya maofisini,na rangi aina ya JOTUN hivyo kwa ajili ya matumizi ya kupaka kwenye majumba na rangi hiyo inatoka nchi za nje hivyo amewataka wananchi kufika banda lao ili kujionea bidhaa hizo.

Amesema kuwa Magare inajihusisha na shughuli za uhandisi wa umeme pamoja na mitambo katika migodini katika viwanda.majumbani na Kampuni nyingine pia katika upande mungine wa uzalishaji ambapo wapo na kampuni Tanzu ya Magare ambayo inazalishaji aina mbalimbali za nguo,viatu,mikanda nk.


Amesema kuwa Magare inatengeza bidhaa hizo katika ubora wa hali ya juu sana hivyo wanawahimiza watanzania kufika na kujionea bidhaa zenye ubora ambazo zinazalishwa nchini na zinatumia mali ghafi ya hapa Tanzania.

Akizungumzia Rangi pamoja na vipande vya ubao ambapo vinaonekana kwenye banda lao amesema kuwa wao ni wasambazaji wa rangi aina Jotun ambayo asili yake ni nchini Norway na imekuwa katika soko takribani miaka 100 hivyo ni moja ya rangi namba moja kwa ubora duniani na nitofauti na rangi ambazo zimezoeleka na watu yenyewe ni rangi ambayo inatopa suluhisho la fuangasi kwenye majumba.


Ameongeza kuwa rangi nyingi siku hizi zinazopakwa kwenye majumba zinapauka kwa haraka sana tofauti na rangi ya Jotun na wananchi wakitembelea kwenye banda lao wataona rangi ambayo inaumri wa hadi miaka 15 na ni rangi ambayo ni suluhisho kwenye kuta zilizo pauka.

"Ndugu waandishi kama mnavyoona hapa kwenye vibao hizi ni demo ambazo zimepakwa kwenye hivi vibao kama sapo ambazo sisi tumekuwa tukipaka kwenye majumba na wito kwa watanzania tupende vya kwetu na kama nilivyosema awali kwamba tunazalisha nguo zenye ubora wa hali ya juu na tumeamua kushindana na kampuni za nje katika kuzalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na bei zetu ni rafiki kwa mtanzania wa hali ya chini"Amesema Kisoi

Nakuongeza kuwa "Tumejikita kwenye nguo za kazi na zenye utepe wa uzuri ambao unaweza kuonyesha hata sehemu za giza kuwa mtu huyo amevaa nguo zenye ubora wa juu na hata unapowauzia watu ,kwamfano tunawauzia watu kutoka nchi tofauti.kama vile Zambia,Jamhuri ya Congo,na hata Kenya hivyo watu waje kwenye banda letu.Amesema.

Amemaliza kwa kusema kuwa baada ya kumalizika kwa maonyesho ya Madini wanapatikana mkoa wa Mwanza maeneo ya City Mall lakini pia bidhaa zinakufikia popote utakapohitaji watakufikia. 


Previous Post Next Post