BOT YAJIPANGA KUANZA KUNUNUA DHAHABU KWA WACHIMBAJI WADOGO WADOGO NA WAKATI



Na Humphrey Msechu, Geita

WAZIRI wa Madini Dkt.Doto Biteko ametembela banda la Benki kuu ya Tanzania lililopo kwenye maonyesho ya tano ya kitaifa ya Teknolojia ya Madini Bombambili mkoani Geita huku akiipongeza Benki hiyo kwa hatua mbalimbali wanazozichukua.

Waziri Dkt Biteko amefurahishwa na namna Benki hiyo ilivyojipanga kufanya kazi kwa ukaribu na wachimbaji wadogo wadogo pamoja na wakati hususani kwa hatua yao ya kutaka kuanza kununua dhahabu moja kwa moja kutoka kwa wachimbaji hao.


Biteko ametoa Pongezi hizo Oktoba 3 mwaka huu katika ufunguzi wa Maonyesho ya Tano ya kitaifa ya Teknolojia ya Madini ambayo yanafanyika katika viwanja hivyo vya Bambambili Mkoani humo. 

"Nawashukuru sana Benki kuu kwa jitihada zenu ambazo mnazifanya ,Asanteni sana."amesema Waziri Biteko.

Na kwaupande wake Meneja Idara ya Mawasialiano kutoka Benki kuu ya Tanzania (BOT) Victoria Msina amesema kuwa Benki hiyo imejipanga kuanza kununua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo na wakati mkoani Geita na hiyo itakuwa njia moja wapo ya kulinda Akiba. 


Amesema kuwa uwepo wao katika maonyesho ya Madini mkoani humo ni njia moja wapo ya kuwaeleza umuhimu wa serikali kuwa na sera muhimu kwa ajili ya mstakabali mpana wa kukuza uchumi wa nchi.

Victoria Ametoa kauli hiyo mbele ya waziri Dkt Biteko alipotembela kwenye banda la Benki Kuuu lililopo kwenye viwanja vya maonyesho ya madini mkoani humo ambapo amesema kuwa wao kama Benki kuu wanajua kuwa kuna wawekezaji wengi katika sekta ya madini hivyo wanapotembela kwenye banda lao wanawafundisha kuhusu kuwekeza katika amana ya serikali.


"kuna umuhimu wa kutumia benki zetu na tunapotumia taasisi za fedha ziko salama na zinasimamiwa vizuri na Benki kuu ya Tanzania na kwasababu wachimbaji wadogo wadogo na wakati wanakuwa hawafahamu noti zetu kwahiyo tunawafundisha noti hizo ili waweze kuelewa alama za usalama zilizopo kwenye noti zetu."


Previous Post Next Post