Brela yawahimiza wajasirimali kurasimisha biashara zao



Na Humphrey Msechu, Geita

AFISA Msajili Msaidizi Brela Bethod Bangahanoze Amewataka wananchi mkoani geita kutembelea kwenye banda la Brela lililopo kwenye Viwanja vya maonyesho ya tano ya teknolojia ya uwekezaji wa madini ili kuweza kurasimisha biashara zao.

Amesema kuwa leo walikuwa wanafanya kazi ya kuzunguka kwenye mabanda kwa lengo la kuwahimiza kufika kwenye banda hilo la brela ili kupata elimu na kuweza kujisajili husani kwa ambao wanafanya biashara zao pasipo kusajiliwa.



Bangahanoze ameyasema hayo septemba 30 mwaka huu mkoani geita kwenye maonyesho hayo ya madini ambayo yanaendelea kwenye viwanja vya Bombambili.ambapo amesema kuwa wafanyabiashara wakishasajiliwa ni rahisi kupata mikopo kwenye taasisi za kifedha kwasababu wanakuwa na dhamana.

"Nawaomba wafanyabiashara ,wajasiliamali kuja kwenye banda letu kurasimisha biashara,na wakirasimisha biashara inakuwa inalindwa kisheria kwasababu ikishasajiliwa hakuna mtu mwingine anaweza kutumia jina la biashara yake na atakuwa nalo yeye pekee yake."Amesema Afisa huyo wa brela


Amesema kuwa kurasimisha jina la biashara gharama zake ni shilingi 20,000, lakini imewanyika mara mbili ambapo shilingi 15000,ni kwa ajili ya usajili na shilingi 5000 kwa ajili ya matunzo na kwaupande wa makampuni inategemea na mitaji yao na nakudai kuwa watu wakitumia maonyesho hayo wataepukana na vishoka.

kwaupande wake mjasiliamali Haika Kawije akizungumzia umuhimu wa kusajili jina la biashara amesema kuwa amepata elimu kutoka brela na kimsingi alikuwa hajasajili jina la kampuni lakini kutokana na elimu aliyoipata atakwenda kusajili na kuhusu gharama ni ya kawaida na anauwezo ya kuilipa.


"Nimefurahi kwa elimu ambayo nimepatiwa na nitaenda kusajili jina la biashara yangu kwasababu kuna faida ya kusajili na kubwa zaidi gharama zake ni nafuu na nitawashawishi wajasiliamali wenzangu waende kusajili."amesema Haika
Previous Post Next Post