WAZIRI MBARAWA- SEKTA YA UCHUKUZI, KULETA MATOKEO CHANYA KATIKA SEKTA NYINGINE ZA KICHUMI NA KIJAMII



Na Lilian Ekonga

Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Sekta ya Uchukuzi  imetengewa jumla ya Shilingi trilioni 2.135 kwa ajili ya kuendeleza na kutekeleza miradi ya kimkakati ambayo itakuwa na matokeo Chanya katika sekta nyingine za kichumi na kijamii.

Hayo yamesemwa Leo jijini Dar es alaam na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amsema  kati ya fedha hizo, Shilingi 94,546,502,000 zimetengwa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 2,041,234,938,000 zimetengea kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo. 

Waziri Mbarawa Amsema Miradi hiyo  ni pamoja na Ujenzi wa Reli ya Standard Gauge (SGR),Ujenzi na ukarabati wa Barabara, Uboreshaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania,  na Ujenzi na Ukarabati wa Meli katika Maziwa Makuu. 




Pia mesema Maeneo mengine yaliyopewa kipaumbele katika mwaka wa fedha 2022/2023 ni pamoja na Ukarabati wa miundombinu ya reli iliyopo, Uboreshaji wa bandari, Uboreshaji wa huduma za usafiri wa anga, maji na nchi kavu,  Uboreshaji wa huduma za hali ya hewa, na uboreshaji wa miundombinu ya kufundishia katika vyuo vya mafunzo ya Sekta za Ujenzi na Uchukuzi.

Aidha Waziri amsema Mradi wa sekta ya uchukuzi unatarajiwa kutoa Ajira Takriban 20,000 huku ujenzi  wa Reli ya SGR kwa kipande Dar Es Salaam – Morogoro, ambao umefikia asilimia 96.76,unataraji kutoa zaidi ya ajira 4,000 zilizo na zisizo za moja kwa moja zitatolewa kwa Watanzania.

"Mwananchi badala ya kutumia takriban saa 12 kwa treli ya kawaida kutoka Dar es Salaam – Dodoma sasa inakadiriwa kuwa mwananchi huyo atatumia saa 4 tu kwa mwendokasi wa Km 160/h".amsema waziri Mbarawa


Pamoja na hayo Waziri amesema Katika mwaka 2022/23, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) imetengewa jumla Shilingi bilioni 100.112 fedha za nje kutoka Benki ya Dunia (WB) na Shilingi bilioni 650.00 kutoka vyanzo vya mapato ya ndani ya Mamlaka kwa ajili ya kutekeleza kazi mbalimbali.


Hata hivyo Amsema Hadi kufikia Mei, 2022, Serikali ilikamilisha ununuzi wa ndege tatu (3) mpya na kuzikabidhi ATCL na kuendelea kutumika.

" Ndege hizo ni Dash 8 Q400 ndege moja (01) yenye uwezo wa kubeba abiria 76 na ndege mbili (2) aina ya Airbus A220-300 zenye uwezo wa kubeba abiria 132 kila moja na  Kuongezeka kwa ndege hizo kumeifanya ATCL kuwa na jumla ya ndege mpya 11 ikilinganishwa na ndege 8 zilizokuwepo mwaka 2020/2021" amsema waziri Mbarawa.

Previous Post Next Post