WATOTO WA KIKE CHANGAMKIENI FURSA YA UMEME



Na Humphrey Msechu Mbeya

MUHITIMU wa mafunzo ya umeme kutoka chuo cha Veta Jijini Mbeya Irene Nduguru amewaasa watoto wakike kuchangamkia fursa ya ufundi umeme ambayo inaonekana kukua kwa kasi sasa hivi nakuondoa dhana ya kuona eneo hilo ni kwa ajili ya watoto wa kiume pekee.

Irene ameyasema hayo julai 2 mwaka huu kwenye maonyesho ya nanenane ambayo kitaifa yanafanyika jijini mbeya chuo cha Veta nimiongoni mwa washiriki katika maonyesho hayo ambapo amesema kuwa yeye ni muhitimu wa mafunzo ya umeme na kwasasa yupo kwenye maonyesho hayo ili kuzungumzia sekta hiyo ya umeme.

Amesema kuwa yeye yupo hapo kwa ajili ya kuonyesha fani yake hiyo ya umeme na mafanikio ambayo ameyapata nakwamba vijana wengi hususani wakike bado wako nyuma katika kujifunza fani hiyo ya umeme lakini kupitia mimi nawahamasisha kusoma umeme na kwaupande wake ilikuwa ni ndoto yake siku moja aje kusoma umeme.


"Nilihamasika kusoma umeme kama mwanamke kwanza niliona kwamba tunapewa kipaumbele sana kwenye kazi za umeme hivyo niliona nichangamkie fursa hii nami kujiendeleza nakwakweli mwitikio ni mzuri na serikali inaendelea kutupa kipaumbele kama wadada."amesema Irene

Ameongeza kuwa tangu amefanikiwa kuhitimu amekuwa akipata kazi japo ndogondogo katika maeneo mbalimbali kwenye makampuni,viwandani na maeneo mengine kiujumla mwitikio mahitaji ni mzuri simbaya  na tangu amehitimu masomo anamiaka nane.

"Tangu nimehitimu nimepata faida nyingi kwaza mimi ni single Mama ,nina watoto wafamilia yangu wananigemea kupitia kazi hii pia nina wazazi ,wadogo zangu lakini pia ninamji wangu na nina kampuni pia hivyo nawahamasisha wanawake waje"amesema 


Amesema anashukuru sana Serikali kwa kujenga Mamlaka hiyo ya Ufundi nchini VETA kwani imekuwa mkombozi kwa vijana wengi wakitanzania na kwakweli vijana wengi wamekuwa wakipata taalumu mbalimbali za ufundi ambazo mwisho wa siku zinakwenda kusaidia maisha yao  na kuweza kusaidia familia zao kwa ujumla.


Previous Post Next Post