URUSI KUWASILI UGANDA KWA MAZUNGUMZO



Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergey Lavrov, anatarajiwa kuwasili Uganda Jumatatu na kuzungumza na Rais Museveni pamoja na viongozi wengine wa serikali.

Urusi imeanza kutafuta uungwaji mkono kwenye masuala yake ya kiusalama kutoka nchi za Afrika baada ya kutokea mapigano kati yake na Ukraine hadi kufikia kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na mataifa ya Ulaya na Marekani.

Taarifa ya Lindah Nabusayi, Katibu Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Rais, Waziri Lavrov atafanya ziara ya siku mbili nchini Uganda.


Previous Post Next Post