Waziri wa elimu Msingi kutoka Afrika ya kusini Mhe.Angeline Moshega (katikati) akizungumza na wanafunzi wenye mahitaji maalumu mara baada ya kutembelea shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko iliyopo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa elimu Msingi kutoka Afrika ya kusini Mhe.Angeline Moshega akiwasili katika viwanja vya shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko na kupokelewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu Mhe.David Silinde Julai 5,2022 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa elimu Msingi kutoka Afrika ya kusini Moshega akiwa pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu Mhe.David Silinde wakishuhudia wanafunzi wenye ulemavu wakionesho uwezo wao wa kutumia kompyuta katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa elimu Msingi kutoka Afrika ya kusini Mhe.Angeline Moshega akiwasili katika viwanja vya shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko na kupokelewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu Mhe.David Silinde Julai 5,2022 Jijini Dar es Salaam.
Na Humphrey Msechu, Dar es salaam
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali na Afrika ya kusini zinatarajia kusaini makubaliano yatakayowezesha wataalamu wa Lugha ya kiswahili kutoka Tanzania kwenda kufundisha lugha hiyo Afrika ya kusini
Mkubaliano hayo yamekuja mara baada ya Waziri wa elimu Msingi kutoka Afrika ya kusini Mhe.Angeline Moshega kutembelea shule ya Msingi uhuru Mchanganyiko iliyopo Jijini Dar es Salaam ambayo inajumuisha wanafunzi wote wakiwemo wenye mahitaji maalumu
Waziri Angeline amesema kusainiwa Kwa makubaliano hayo kutasaidia nchi hizo mbili kubadilishana uzoefu na utaalamu wa namna ya kufundisha walimu pamoja na kushirikiana kwenye kuiboresha Mitaala ya elimu ya nchi hizo.
Nae Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu Mhe.David Silinde amesema makubaliano hayo ni fursa Kwa Tanzania kutoa wataalam wa lugha kwenda kufundisha Afrika ya kusini lakimi pia italeta tija kweny ukuajibwa uchumi
Aidha Mhe. Silinde amesema kupitia makubaliano hayo Tanzania inaangalia uwezekano wa kuanza kutoa elimu ya lugha ya alama kama ilivyo Kwa taifa ya Afrika ya kusini