SERIKALI YAWATAKA VIJANA KUTAMBUA VIPAJI VYAO WAKIWA BADO CHUONI


Serikali imewataka  vijana wa Kitanzania hususani wa  Elimu ya juu nchini kutambua vipaji vyao wakiwa bado Chuoni ili kufikia malengo waliojiwekea kupitia vikundi vya ujasirimali nakuleta tija kwenye jamii inayowazunguka.

Akizunguza wakati wa Hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Mzalendo Project Foundation tawi la Chuo Kikuu Cha Afya Shirikishi Cha Muhimbili MUHAS,Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Patrobas Katamb ,amesema serikali imekuwa ikijenga mazingira wezeshi kwa vijana kujikwamua kiuchumi hivyo kuwataka kutumia fursa hiyo kubadilindoto zao Kwa ustawi wa taifa lao.

Naibu Waziri amesema Serikali ya Awamu ya sita ipo Tayari kuweza kuunga mkono na kuhakikisha vijana wanapata msahada wa mitaji Ili waweze kunikwamia kiuchumi.



"Vijana kama Hawa Wamekuwa na malengo mahususi ya kujiandaa kabla hawajamaliza chuo kikuu  na namna ya kujiajiri na Kupata fursa mbalimbali"amesema Naibu Waziri.

Aidha Naibu Waziri Katambi amesema vijana wajitambue na wawe na ndoto na shabaha baada ya Hapo Serikali itatengeneza mazingira wezeshi ya kujitambua na Changamoto za kiuchumi.


Pia Amesema vijana ni nguvu kazi ya Taifa hivyo wanaapswa kujipambanua kwenye fursa zinazo wazunguka Ili kufikia malengo waliyojiwekea.

"Uwepo WA Techonolojia mpya umepunguza Ajira hivyo hupelekea idadi  kubwa ya uchache wa Ajira kwa vijana" Amsema Naibu Waziri Katambi.



Previous Post Next Post