Magari 633 yalikamatwa na madereva 166 waliandikiwa faini, madereva 14 walipelekwa mahakamani, madereva 102 walionywa na kupewa elimu, magari 12 yalizuiliwa kutembea barabarani kutokana na ubovu uliokithiri, na kesi 62 bado zinaendelea na upelelezi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri ya ndani nchi
Mhe Jumanne Abdallah Sagini wakati akizungumza na Waandishi wahabari kufutia operesheni kubwa ya kuyakamata magari na kuwachukulia madereva hatua mbalimbali za Kisheria kwa makosa mbalimbali ya usalama barabarani.
Naibu Waziri Jumanne Amsema Tathmini iliyofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wadau wengine wa usalama barabarani imebaini kuwa, ajali za barabarani husababishwa na mambo kadhaa yakiwemo makosa ya kibinadamu, ubovu wa vyombo vya moto na miundombinu ya barabara huku makosa ya kibinadamu yameonekana kuchangia asilimia 80 ya ajali hizo.
"Katika kipindi cha hivi karibuni, yamejitokeza matukio ya ajali mbaya za magari zilizosababisha vifo na majeruhi wengi kwa wakati mmoja, uharibifu wa mali, hususani katika Mikoa ya Iringa, Simiyu na Kagera. Katika matukio hayo watu walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa pamoja na uharibifu wa magari hayo na Ajali hizo zimefanyiwa uchunguzi na hatua mbalimbali za Kisheria zimechukuliwa kwa wahusika"amesema Naibu Waziri.
Aidha Amesema kutokana na Matukiao Hayo serikali imeelekeza mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) wakae pamoja na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani na kupitia idadi ya magari madogo yaliyopewa leseni za biashara ya kusafirisha abiria kutoka eneo moja kwenda lingine na kutathimini ukiukwaji wa masharti ya leseni kisha kuwachukulia hatua za kisheria madereva na wamiliki waliokiuka masharti ya leseni zao.
Pia ameelekeza Jeshi la Polisi liendelee kufanya ukaguzi endelevu wa magari yote na yale yatokayobainika kuwa na ubovu unaoweza kuhatarisha maisha ya watu na mali zao wasiruhusiwe kuendelea kutembea barabarani hadi yatakapofanyiwa matengenezo stahiki.
"Serikali inawashauri wafanyabiashara wenye uwezo waombe leseni za usafirishaji wa abiria kutoka LATRA kwenye maeneo yenye uhitaji yakiwemo Mikoa ya Simiyu, Kagera, Kigoma, Mara, Geita na kwingineko" amesema Naibu Waziri.
Hata hivyo Naibu Waziri amewaomba Wamiliki wa vyombo vya moto waliopata leseni za usafirishaji wa abiria, waendelee kusafirisha abiria kwa kuzingatia masharti ya leseni zao.