Na Lilian,
Katika hali ya kushtusha, Msanii wa filamu nchini Tanzania Farida Sabu maarufu kwa jina la 'Bi Sonia' amefariki dunia.
Muigizaji huyo ambaye alijulikana sana kupitia kikundi cha Kole Sanaa group amefariki leo, mjini Zanzibar ambapo alikuwa anauguzwa na mwanae.
Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji, Chiki Mchoma amethibitisha taarifa hizo, huku msiba ukitarajiwa kufanyika huko huko Zanzibar.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Apumzike kwa amani