MAMA ASIMULIA KAULI YA MWISHO YA WATOTO WAKE WALIOFARIKI KWENYE AJALI MTWARA


“Bye dady, bye mamy.” Hayo ndio maneno ya mwisho waliyoyatoa watoto wawili wa familia moja waliofariki dunia katika ajali ya basi iliyoua watu 11 wakiwamo wanafunzi tisa, wakiwaaga wazazi wao kabla ya kuondoka nyumbani kwenda shuleni.

Akisimulia kwa uchungu, Stella Yohanna ambaye ni mama wa watoto hao wawili amesema kuwa hiyo ndio ilikuwa tabia yao na asubuhi baada ya kuwaanda walikwenda kumuaga baba yao kabla ya mama huyo kuwapeleka kwenye gari la Shule ya Msingi ya King David.

Stella ambaye ni mkazi wa Mtwara mjini amepoteza watoto wake wawili katika ajali hiyo ambayo imetokea asubuhi leo Jumanne Julai 26, 2022 eneo la Mjimwema, Kata ya Mikindani, Mtwara Mjini wakati watoto wakipelekwa shuleni.





Previous Post Next Post