HAJI MANARA ALAMBA DILI NONO KUTOKA BAYPORT

 


Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services Ltd imemtangaza Afisa Habari wa  klabu ya Yanga Haji Manara kuwa balozi wake kwa ajili ya kufanya kazi pamoja.

Akizungumza katika hafla fupi ya kutiliana saini na kumtangaza rasmi katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam, Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Bayport Financial Services Ltd bwana Nderingo Materu amesema lengo la taasisi hiyo kumpatia mkataba huo ni  kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufikisha ujumbe pamoja na ushawishi wake kwa jamii.

“Haji Manara wote ni mashahidi amefanya mambo makubwa sana, hivyo tumeamua kumshirikisha katika hili kwa sababu tunaamini atakuwa Balozi mzuri kwetu kwa kusaidia kufikisha ujumbe wa Taasisi yetu kwa wateja wetu,” Alisema Materu.

Alisema katika kipindi cha miaka 16 tangu kuanza rasmi shughuli zake nchini tayali wamefanya mambo makubwa, kwa sasa taasisi yetu  wamejikita zaidi katika kutoa mikopo kwa watumishi wa umma kwa njia ya kidigitali.

"Mtumishi wa umma anaweza kupata mkopo kwa njia ya kidigitali ndani ya masaa 24 jambo ambalo linasaidia kuokoa muda kutokana na mteja kutolazimika kufika ofisini wala kujaza fomu". Alibainisha bw Materu.

Kwa upande balozi mteule taasisi hiyo bwana Haji Manara ameahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwa Taasisi ili kuhakikisha inafikia malengo yake.

“Nianze kwa kushukuru Bayport Financial Services kwa heshima na imani kubwa walionayo kwangu na familia yangu, ni heshima kwa Taasisi yangu ya Yanga na Tasnia ya Mpira wa Miguu ambayo nimeitumikia kwa muda mrefu,”Alisema Manara

Wote ni mashahidi sina jambo dogo,
Bayport Financial Services ni taasisi inayofanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) nitafanya kazi kwa uweledi, na kwa ushirikiano mkubwa katika kipindi chote cha mkataba huu, kufikia malengo
Previous Post Next Post