SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LAINGIA MAKUBALIANO YA KIBIASHARA NA KAMPUNI YA USAFIRISHAJI TUTUME KATIKA USAFIRISHAJI WA SAMPULI ZA KIBAIOLOJIA



Serikali kupitia wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, imesema itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kutekeleza huduma ambazo zitawafikia wananchi moja kwa moja.

Kauli hiyo imetolewa leo na waziri Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya biashara ya usafirishaji wa sampuli za kibaiolojia baina ya shirika la posta nchini -TPC na kampuni ya usafirishaji -TUTUME.



Waziri Nape amesema serikali inatambua na kuthimini mchango wa sekta binafsi, hivyo ushirikiano huo utasaidia kurahisisha upatikanaji wa sampuli huku akilitaka shirika hilo kuangalia uwezekano wa kushirikiana na wadau wa kilimo hasa katika usafirishaji wa mbegu.

Kwa upande wake, Posta Masta Mkuu wa shirika la Posta nchini -TPC, Macrice Mbodo amesema ushirikiano huo utasaidia kurahisisha usafirishaji wa sampuli za magonjwa katika vituo vya afya ngazi kwanza hadi ya pili.



Naye, Mkurugenzi mkuu wa shirika la usafirishaji -TUTUME, Misana Manyama amesema watatumia fursa hiyo katika utekelezaji wa majukumu pamoja na kuongeza ajira kwa vijana hasa madereva wa pikipiki

Hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo yameshuhudiwa na viongozi mbalimbali wa serikali ikiwa ni pamoja na katibu mkuu wizara ya habari, mawasiliano na teknolojia ya habari Dkt Jimmy Yonazi, Mwenyekiti wa Bodi -TPC, Mwakilishi wa katibu mkuu kutoka wizara ya Afya Dkt John Mombeki.
Previous Post Next Post