CHUO CHA TAKWIMU CHA AFRIKA MASHARIKI CHA FUNGUA MAFUNZO YA AWAMU YA PILI WASIMAMIZI TEHAMA SENSA YA MAKAZI NA WATU 2022



Chuo cha Takwimu Cha afrika Mashariki kimefungua mafunzo ya pili ya Wasimamizi wakuu wa Tehama kwa ajili ya Sensa na Makazi ya Watu itakayofanyika tarehe 23 mwezi wa nane mwaka huu 2022.

Akizungumza katika ufunguzi huo Mwenyekiti wa Bodi Chuo cha Takwimu afrika Masharik Prof. Ahmed Ame amesema kuwa mafunzo haya yatakuwa ni ya siku tano na yatajumuisha jumla ya washiriki 119 kutoka Tanzania Bara na Visiwani ( Zanzibar )


"Unajua Sensa ya sasa hivi imebadilika tofauti na zamani, Zamani Wasimamizi wa Sensa walikuwa ni wa Takwimu au Watu wa maswala ya mipango, sasa hivi Dunia imebadilika Wasimamizi wa 
Sensa ni watu wa IT" Alisema Prof. Ahmed Ame



Kwa upande mwingine Mkuu wa chuo hicho Dkt. Tumain Katunzi amesema kuwa Wasimamizi hawa wa Tehama kwa upande wa Sensa wanafundishwa mbinu mbalimbali za kusimamia na kukusanya Takwimu za Sensa hiyo.



Previous Post Next Post