TAASISI YA USTAWI WA JAMII YATOA WITO KWA VYUO VIKUU KUFANYA TAFITI KWA NJIA YA MADODOSO NA MAHOJIANO



Taasisi ya Ustawi wa Jamii imetoa wito kwa Vyuo vikuu na vya Kati kufanya Utafiti kwa kutumia njia ya Madodoso na Mahojiano ili kupata Takwimu sahihi za Matukio ya Ukatili wa Kingono kwa Wanafunzi wa Vyuo hivyo na Jamii kwa Ujumla.

Wito huo umetolewa na Na Naibu Mkuu wa Chuo, Kitendo Cha Fedha na Mipango Profesa Justice Urassa katika Mkutano wa Ufanyaji wa Tafuti za Kupinga Ukatili wa Kingono kwenye Mitandao ya Kijamii.

Profesa Urassa amesema Utafiti huo wa kutumia Mitandao ya Kijamii Kupinga Ukatili wa Kingono kwa Wanafunzi ni Muhimu kwenye Nchi ya Tanzania kweni kumekuwa na ongezeko na Matukio hayo yanayowapata Wanafunzi wawapi Mashuleni.


Aidha, Ametoa wito kwa Wanafunzi kutumia  Madawati ya kijinsia yaliyopo vyuoni kupata ushauri Nasaha pale anapotendewa Ukatili wa Kijinsia na kuachana na kutumia Watu ambao hawana Weledi wa Kutoa Ushauri huo Hali inayoweza kusababisha Kushawishika kufanya Vitendo visivyofaa.

Naye Mtafiti katika Chuo Cha Ustawi wa Jamii Itika Gwamaka, amesema Utafiti huo umelenga Wanafunzi pamoja na Jamii kwani Vitendo hivyo viko kwenye Jamii Huku Akitoa wito kwa Vyombo vya Habari kuendelea Kupinga Vitendo vya Ukatili wa kijinsia kupitia vipindi mbalimbali na Kutoa Elimu kwa Jamii kuhusu Athari za Vitendo hivyo
Previous Post Next Post