Mkuu wa Wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe ameitaka jamii kuwathamini watu wenye mahitaji Maalumu ikiwemo wasioona,walemavu wa ngozi wasio na viungo kwani nao wanapaswa kupatiwa haki kama watu wengine.
DC Gondwe ametoa rai hiyo wakati wa tamasha la Watoto wenye Mahitaji Maalumu lililoandaliwa na Kijiji cha Makumbusho ya Taifa lenye ujumbe usemao"Haki Sawa Kwa Wote" lengo ni kuwakutanisha Watoto wenye Ulemavu wa aina mabalimbali ikiwemo ulemavu wa viungo na walemavu wa ngozi( Albino).
Aidha amesema kwamba Watoto wenye ulemavu wanatakiwa,kutambuliwa, kuthaminiwa na kupatiwa haki zao za msingi ikiwemo elimu ili kuwafanya waweze kuishi katika maisha bora ,huku akikemea jamii kuacha vitendo vya unyanyapaa kwa Watoto hao.
Sanjari na hayo amekipongezs Kijiji cha Makumbusho ya Taifa kwa kuandaa tamasha hili ambalo limelenga kutambua thamani ya Watoto wenye ulemavu,natoa wito kwa jamii,taasisi na mashirika mbalimbali kuendelea kuwathamini watu wenye ulemavu" amesema DC Gondwe.
Watoto wenye ulemavu kutoka shule mbalimbali za msingi ikiwemo shule ya Mgabe,Shule ya Msingi mchanganyiko,Shule ya Msingi Jeshi la Wokovu ,wamekutana kwenye tamasha hilo nakuweza kushiriki Mambo mbalimbali ikiwemo michezo na burudani.
Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Kijiji cha Makumbusho Bi.Wilhelmina Joseph amesema kwamba Makumbusho ya Taifa itaendelea kuthamini makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo Watoto wenye mahitaji mbalimbali ili kuwafanya wapate haki zao za msingi.
"Aidha amesema Wameandaa tamasha hilo ili kuthamini haki za Watoto hawa ,hivyo sisi Kama Makumbusho ya Taifa na tamasha hilo la Watoto wenye mahitaji Maalumu na wamewe kauli mbiu ya Haki Sawa kwa Wote" ili kuifanya jamii itambue kuwa hata watu wenye ulemavu wana haki sawa na wengine hivyo wasiwafiche majumbani" amesema Bi Wilhelmina.
Akizungumza kwa niaba ya Walimu Wenzake kutoka shule hizo Bw.Emanuel Ibrahim kutoka shule ya Msingi ya Jeshi la Wokovu ( Salvation Army) amesema kwamba ulemavu siyo kushindwa hivyo wameiomba Makumbusho ya Taifa kulifanya tamasha hilo kuwa endelevu kwani Watoto wanafurahia kuwa na wao wanathaminiwa.