TALGWU YAKANUSHA TAARIFA ILIYOTOLEWA NA GAZETI LA JAMUHURI "TUTAWAFUNGULIA KESI MAHAKAMANI".


Chama Cha Wafanyakazi wa serikali za Mitaa Tanzania(TALGWU), kimekanusha  taarifa zilizo tolewa na Gazeti la Jamuhuri kuhusu kupigwa kwa Fedha za chama kwenye zabuni ya kutengeneza Sare za Mei Mosi 2022 na Utata wa Manunuzi ya Gari za TALGWU katika chapisho  la Tarehe 10 mwezi Mei yenye kichwa Cha Habari FEDHA ZA TALGWU ZA PIGWA

Akizungumza na waandishi wa Habari Katibu  Mkuu wa TALGWU, Rashid Mtima amsema  kutokana upotoshaji huo watalishitaki na kulifungulia Kesi Mahakamani  Gazeti la Jamuhuri kutokana na taarifa hiyo Ambayo imezua taharuki kwa wanachama na wadau wengine wa TALGWU.

Amsema Gazeti la Jamuhuri liliripoti kwamba katika zabuni ya Sare za Mei mosi za mwaja 2019 kulikuwa na udangangangifu kwa kutengeneza Sare 60,000 lakin malipo yaliyofanyika ni Sare 80000 na kofia hazikipelekwa jambo lililolzimu mikoa kununua kofia za wanachama.



"Huu ni upotoshaji na uongo uliokithiri wenye dhamira ovu ya kuichafua TALGWU na uongozi wake kwani ukweli ni kwamba ununuzi wa sare.za Mei mosi 2019 uligharibu kiasi Cha Shilingi 934, 560,000 kwa idadi ya fulana 80000 na kofia 80,000 na haijawahi kutokea ofisi za Mikoa zikakosa kofia na kujinunulia zenyewe". amesema  Katibu.

Aidha Amesema siku ya jumanne  ya Tarehe 24 Mei 2022 Gazeti ja Jamuhuri katika ukurasa wakewa kwanza, wa tatu na watano ilichapisha habari yenye kichwa Cha  Habari, UTATA UNUNUZI MAGARI TALGWU huku likiwa na lengo la kuendelea kuichafua TALGWU  na kuzua taharuki kwa wanachama wake bila sababu za zozote za msingi.

Haya hivyo amesema Manunuzi yoyote ya TALGWU  yanazingatia kanununi za maunuzi ya chama toleo la mwaka 2018 pamoja na bajeti ya Chama inayopitishwa na Baraza Kuu la Chama Taifa, hivyo taarifa iliyoandikwa katika Gazeti la Jamuhuri kwamba Kuna Utata katika ununuzi wa magari ya TALGWU imepotosha Umma kuhusu ukweli halisi wa suala Hilo.

TALGWU inawaasa waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa weledi na kuzingatia taaluma na maadili ya uandishi wa habari Ili kuhakikisha kuwa wanaandika habari za ukweli za kutopotosha Umma na kuharibu taswira ya taasisi.



Previous Post Next Post