LHRC YATAO TAMKO LA KULAANI TUKIO LA JARIBIO LA KUTAKA KUKATWA MKONO MTU MWENYE UALBINO..


Kituo Cha Sheria na Haki za binadamu (LHRC) kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kunusurika kukatwa mikono kwa ndugu Mohamed Rajabu mwenye ualbino  mkazi wa kata ya Mabibo jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi Mtendaji wa (LHRC) Anna Henga Amesema Ndugu, Mohamed Rajabu alishambuliwa tarehe 25 April 2022 na watu wasiojulikana waliokuwa na lengo la kumkata mikono yake.

"Kwa Mujibu wa Mashuhuda wakiwemo wanafamilia wakiwemo wanafamilia wamesema wahalifu hao walijaribu kutaka kumkata mikono yake kitendo ambacho hakikufanikiwa, hata hivyo walifanikiwa kumjerihi Mohamed Rajabu kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake"amesema Anna Henga.



Aidha kituo Cha Sheria na Haki za binadamu kimetoa with kwa Jeshi la Polisi na serikali kuhakikisha kuwa watuhumiwa wa KESI hii wanakamatwa , upepelezi inafanyika kwa wakati na kufikisha mahakamani na kupatiwa adhabu Kali Ili iwe fundisho kwa watu wengine.

Pia wameliomba Jeshi la polisi Kupanua upepelezi wa Kesi hizi Ili kukamata wahamasishaji wa soko hili haramu la viungo vya watu wenye ualbino, ambao ni waganga wa kienyeji na wanoamini Imani za kishirikina Ili wachukuliwe hatua Kali za kisheria.

Kituo Cha Haki za Binadamu kinapenda kutambua juhudi ambazo serikali imezifanya Ili kupatikana kwa Mpango kazi wa taifa wa watu wenye ualbino.



Previous Post Next Post