Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Kassim Majaliwa amepongeza jitihada zinazofanywa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika kukuza Sanaa ya muziki na kuitangaza Tanzania kupitia Tamasha la Muziki la Serengeti.
Mhe. Majaliwa ametoa kauli hiyo leo kupitia simu ya Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi ambapo amefafanua kuwa Serikali inaunga mkono jitihada hizo na kwamba tamasha hili litaendelea kuboreshwa zaidi mwakani ili lengo lake liweze kufikiwa.
Pia amesema kupitia Tamasha hili Rais wa Jamhuri ya Muungano anawasalimu na kuwapongeza wasanii kwa kazi nzuri wanazofanya katika kuitangaza Tanzania.
Aidha, amemwelekeza Katibu Mkuu. Dkt, Hassan Abbasi kusimamia kufanya tathimini ya Tamasha hili ili kubaini changamoto ili zisaidie kuboresha tamasha la mwakani.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Pauline Gekul amemshukuru Mhe. Waziri Mkuu na amemhakikishia kuendelea kutekeleza maelekezo yote kwa faida ya wasanii wa Tanzania.
Tamasha hili limedhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa Serikali, wabunge na Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Dodoma. Mhe, Antony Mavunde.
Tamasha hili ni la siku mbili Machi 12 na 13, 2022 na linatarajiwa kuwapandisha wasanii takribani 200.



