MFUMUKO WA BEI ZA BIDHAA UMEPUNGUA KUTOKA ASILIMA ASILIMA 4.0 MPAKA ASILIMIA 3.7.


Ofisi ya taifa ya Takwinu imetoa mfumuko wa Bei wa Taifa unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari,  Kaimu Mkurugenzi  wa sensa ya watu na makazi Ruth Minja, Amesema mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi FEBRUARI, 2022 umepungua hadi asilimia 3.7 kutoka asilimia 4.0 ilivyokuwa kwa mwaka ulioishio mwezi JANUARI, 2022. 

"hii inamaanishakuwa, kasiya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi FEBRUARI,2022 imepunguaikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mweziJANUARI, 2022". amesema Ruth Minja

Aidha amesmea Kupungua kwa Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi FEBRUARI, 2022 kumechangiwa na kupungua kwa Mfumuko
wa bei wa baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi FEBRUARI, 2022 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka ulioishia mwezi JANUARI, 2022.

Amesma Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoonesha kupungua kwa Mfumuko wa bei kwa mwaka  ulioishi mwezi FEBRUARI 2022 ikilonganishwa na mwaka ulioishia mwezi mwezi JANUARI ,2022 ni pamoja na  matunda (kutoka
asilimia 9.5 hadi asilimia 5.2); mbogamboga (kutoka asilimia 5.0 hadi asilimia 3.7): kunde (kutoka asilimia 7.1hadi asilimia 2.0); njegere (kutoka asilimia 6.8 hadi asilimia 4.2); siagi (kutoka asilimia 6.6 hadi asilimia 6.5);tambi (kutoka asilimia 4.2 hadi asilimia 3.9) na bidhaa nyingine za ngano za kuoka (kutoka asilimia 8.4 hadi  asilimia 5.8).

"Kwabupande mwingine, baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoonesha kupungua kwa Mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi FEBRUARI, 2022 ikilinganishwa na mwaka ulioishia mwezi JANUARI, 2022 ni pamoja na: nguo za watoto kutoka asilimia 3.5 hadi asilimia 2.9); mkaa (kutoka asilimia 6.4 hadi asilimia 6.1);
magodoro (kutoka asilimia 7.3 hadi asilimia 6.2) na huduma ya vyakula kwenye migahawa (kutoka asilimia 2.7hadi asilimia 1.9)" amesema Kaimu Mkurugenzi.

Amesema Kwa ujumla, Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwaka ulioishia mwezi FEBRUARI, 2022 umepungua hadi asilimia 6.1 kutoka asilimia 6.3 kwa mwaka ulioishia mwezi JANUARI,2022.



Mfumuko wa bei ambao haujumuishi bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi FEBRUARI, 2022 nao umepungua hadi asilimia 2.7 kutoka asilimia 3.1 ilivyokuwa kwa mwaka ulioshia mwezi JANUARI, 2022.

Kwa upande wa hali ya Mfumuko wa Bei kwa Bidhaa ya nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka ulioishia mwezi February 2022 Nchini Uganda, Mfumuko wa Bei kwa mwaka ulioishia mwezi FEBRUARI, 2022 umeongezeka hadi asilimia 3.2 kutoka asilimia 2.7 kwa mwaka ulioishia mwezi JANUARI, 2022. Kwa upande wa Kenya, Mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi FEBRUARI, 2022 umepungua hadi asilimia 5.08 kutoka asilimia 5.39 kwa mwaka ulioishia mwezi JANUARI, 2022.
Previous Post Next Post