AIRTEL KWA KUSHIRIKIANA NA MKUU WA WILAYA YA RUKWA WAKABIDHI MSAADA KWENYE KITUO CHA WATOTO YATIMA

        

Mkuu wa wilaya ya sumbawanga SEBASTIAN WARYUBA amewataka wananchi kujitoa kwa moyo mmoja kuwasaidia watoto wenye mazingira hatarishi ili kuondoa adha ya watoto kuzura ovyo mtaani .

Ameyasema hayo wakati wa kukabidhi zawadi ya mwaka mpya katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Katandala zilizotelewa na kampuni ya Airtel ili kufurahi kwa pamoja na watoto hao.




Hata hivyo meneja wa @airtel_tanzania wa kanda ya RUKWA amesema hilo jambo la kutoa misaada kwa watoto yatima ni kila mwaka kampuni inafanya hivyo na mwaka huu wameanza kwa kutoa zawadi zenye gharama kiasi cha shilingi milioni moja na nusu katika kituo cha watoto yatima katandala.




Kwa upande wao Msimamizi wa kituo hicho cha kulelea watoto yatima cha katandala Sister Lucy Maganga ametoa wito kwa jamii kuweza kujitoa kuwasaidia watoto hao kwa sababu hawana wazazi wa kuwalea.

"Kuwalea watoto yatima ni jukumu letu sote watanzania na pia tuendelee kujitoa kwa hilo ili tupunguze mimba na ndoa za utotoni kwa mkoa wa Rukwa"

  #sparklight_tvupdates #sparklight_tv


Previous Post Next Post