Jumuhiya ya wanataaluma wa kiislamu Tanzania ( TAMPRO) imefanya mkutano wa mwaka jijini Dar es Salaam na kubainisha mambo matano wanayotarajia kuyafanya katika miaka minne ya uongozi wao ambayo yatakuwa ni dira ya maendeleo kwa kipindi hicho.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Mwenyekiti wa TAMPRO, Haji Mrisho amesema mambo yanayotarajiwa kufanyika katika kipindi hicho ni kufanya tafiti Ili kuleta masuluhisho ya changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili jamii.
Pia amesema watatoa ushauri wa kitaalamu, kujenga uwezo kwa kupitia mafunzo na kufanya kushawishi na utetezi kwa maana ya kwamba kufanya utetezi katika njia ya kitaalamu hasa kuepusha mambo ambayo yanaweza yakaleta migogoro katika jamii.
Mwenyekiti huyo Aliongeza kuwa katika mikakati hiyo pia wanatarajia kuanzisha Miradi uchumi.
Mbali na yako mwenyekiti huyo amesema mambo ambayo wataendelea kudumu nayo ambayo walikua wakiyafanya ni kujenga ushirikiano na mahusiano na Taasisi na wadau wa maendeleo ikiwemo serikali.
Pia mwenyekiti wa TAMPRO alitoa wito kwa wataalamu wote kufanya kazi kwa weledi na kuleta masuluhisho ya changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili jamii;
“Wito kwa wataalamu kufanya kazi kwa weledi iwe kazi ya mfano ili watu waweze kujifunza na awe wakala wa mabadiliko kuleta masuluhisho ya matatizo ya wananchi ambayo wanayo”