RC SONGWE AVUTIWA NA TEKNOLOJIA ZA UDOM KUTATUA CHANGAMOTO ZA JAMII





Na   Lilian Ekonga, Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabiri Omari Makame, ameipongeza Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa hatua kubwa iliyopiga katika utafiti na ubunifu, akisema tafiti zinazofanywa na chuo hicho zimekuwa zikitoa majawabu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.

Makame amesema hayo Agosti 7, 2026, baada ya kutembelea banda la UDOM katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Samwel Malecela, Nzuguni, jijini Dodoma, ambapo alieleza kufurahishwa na bunifu mbalimbali zilizooneshwa na chuo hicho.

Amesema moja ya mambo yaliyomvutia ni namna UDOM inavyotumia tafiti na teknolojia kutatua changamoto katika sekta mbalimbali, ikiwemo kilimo, afya na bima.

“Nimeona mambo mengi sana ya uvumbuzi katika teknolojia ambayo yanatoa majawabu kwenye changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikikabili jamii,” amesema Makame.

Ameeleza kuwa miongoni mwa bunifu alizoziona ni teknolojia inayoweza kubaini mahitaji ya maji kwenye udongo na kuwezesha mfumo wa umwagiliaji kufanya kazi moja kwa moja kulingana na hali ya udongo, hatua ambayo inaweza kumsaidia mkulima kutumia maji kwa ufanisi zaidi.




Aidha, amesema amevutiwa na ubunifu wa ‘White Box’ kwa magari, mfumo unaoweza kukusanya taarifa muhimu wakati wa kutokea kwa ajali, ikiwemo kasi ya gari na mazingira yaliyosababisha ajali, akisema teknolojia hiyo inaweza kusaidia wataalamu katika uchunguzi wa ajali na sekta ya bima.

Makame pia ametaja bunifu za UDOM katika eneo la afya, ikiwemo utafiti wa bidhaa zinazolenga kutatua changamoto za kiafya, akisisitiza kuwa ubunifu huo unaonesha umuhimu wa vyuo vikuu kuunganisha taaluma na mahitaji halisi ya jamii. 

Kwa upande wake, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Fedha, Mipango na Utawala wa UDOM, Profesa Jeifta Sunzu, amesema ushiriki wa Chuo Kikuu cha Dodoma katika Maonesho ya Nanenane unalenga kuwaonesha wananchi kazi mbalimbali za utafiti, ubunifu na teknolojia zinazofanywa na chuo hicho kwa ajili ya kutatua changamoto na kuleta manufaa kwa Watanzania.



Amesema UDOM imeendelea kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia kwa kuandaa mitaala mipya inayohusu Akili Unde (Artificial Intelligence), ambayo tayari imewasilishwa na kuidhinishwa na mamlaka husika.                                 


H




Previous Post Next Post