Na mwandishi wetu…
Mgombea ubunge wa Jimbo la Kigamboni kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Wakili Mwanaisha Mndeme, ameendelea na kampeni zake kwa mfumo wa “Mtaa kwa Mtaa” katika Kata ya Somangila.Wakili Mndeme aliambatana na Mgombea Udiwani wa Kata hiyo ya Somangila kupitia ACT Wazalendo Ndugu Salumu Liwanda.
Katika kampeni hizo, Wakili @mwanaisha__mndeme ameahidi kushughulikia changamoto zinazowakabili wakazi wa Kigamboni endapo atachaguliwa kuwa Mbunge, akitaja maeneo ya kipaumbele kuwa ni Miundombinu ya barabara, huduma za vivuko,ajira,elimu na Afya.
Aidha, amesema kuwa Kigamboni ni eneo lenye fursa nyingi lakini limekosa usimamizi mzuri wa kisera, jambo ambalo limechangia wananchi wengi kuendelea kukumbwa na umasikini na ukosefu wa huduma bora za kijamii.
Kupitia kampeni hiyo ya mtaa kwa mtaa ,Wananchi wa Jimbo la Kigamboni walitumia fursa hiyo kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili, huku wengi wakionesha matumaini kwa mgombea huyo kuleta mabadiliko endapo atapewa nafasi ya kuwaongoza.