ALIYEKUWA KIONGOZI WA BAWACHA, SIGRADA MLIGO, ATANGAZA KUJIUNGA NA CHAUMA

 




Na Mwandishi wetu....

Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA)taifa, Bi. Sigrada Mligo, ametangaza kujiondoa rasmi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akilalamikia kile alichokiita kauli za kubeza mchango wake na mazingira ya “unyanyasaji wa ndani ya chama.” 

Akizungumza na wanahabari siku ya Jumatatu katika makao makuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Kinondoni jijini Dar es Salaam, Bi. Mligo amesema kuwa ameumizwa na namna anavyotajwa kuwa chanzo cha migogoro, licha ya kuwa mmoja wa waliokibeba chama wakati wa kipindi kigumu. “Mwaka 2019 tuliendesha CHADEMA Digital ambayo ilikuwa inasajili wanachama na kushughulikia masuala ya uchaguzi. 

Lakini kwenye uchaguzi wa Januari 2025, CHADEMA ilishindwa kufanya operesheni kwenye majimbo ya Makete, Wang’ing’ombe na Ludewa kwa sababu ya ukosefu wa bajeti. 




Mimi ndiye nilimpigia Katibu Mkuu Mnyika kuuliza sababu, na yeye akathibitisha kuwa hawana fedha,” amesema Mligo. 

Kwa mujibu wa Mligo, aliamua kufadhili operesheni hiyo kwa fedha zake binafsi, akitumia zaidi ya shilingi milioni 15 kuhakikisha kuwa majimbo hayo matatu katika Mkoa wa Njombe yanashiriki mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama. 


“Niliigharamia kwa fedha zangu hadi majimbo yanapata uongozi ambao ulipiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa chama. Zipo kwenye kumbukumbu rasmi, hawawezi kubisha,” amesisitiza. Hata hivyo, Sigrada alisema licha ya kujitolea kwake kwa hali na mali, amekuwa akidhihakiwa na baadhi ya wanachama na viongozi wa CHADEMA ambao, kwa maneno yake, wanajifanya kuwa wao ndio waliokifia chama kuliko wengine. 


“Sasa unakutana na lugha za kienyeji sana ambazo zinataka kuonesha kwamba kuna watu wameipambania CHADEMA, kuna watu wameifia CHADEMA kuliko watu wengine, kwahiyo sisi watu wengine sio watu wa matangazo na siyo watu wa mitandaoni, ndiyo maana nikasema nikisema niliyoyafanya kwenye chama hiki halafu mtu anakuja na lugha laini kwamba Sigrada anakiua chama, unamshangaa”, ameeleza Sigrada. 


Kauli ya Mligo imekuja miezi kadhaa baada ya kuripotiwa kujeruhiwa na mmoja wa walinzi wa CHADEMA wakati wa kikao cha ndani kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, 
Previous Post Next Post