AIRTEL Tanzania imezindua huduma ya kadi ya Malipo ya Kidigitali ‘Airtel Money Global Pay ili kuwawezesha watanzania kufanya Malipo ya huduma mbali mbali Kitaifa na Kimataifa
Akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma hiyo Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Money Adolph Kasegenya amesema Airtel Money Global Pay ni huduma ya Malipo itakayoiwezesha jamii ya kitanzania kufanya malipo Kidigitali ndani na nje ya nchi bila usumbufu
Amesema kadi hii ya kidigitali itawaeezesha na kuwarahisishia watanzania kulipia bidhaa au huduma kwenye majukwaa ya kimataifa kwa ajili ya masomo manunuzi ,safari au burudani kipitia simu zao za mkononi
Amesema kadi hii inapatikana kipitia programu ya MyAirtel App na kwamba ni salama kwa matumizi na pia watumiaji watapata usalama na uharaka wa malipo yao na kwamba huduma hii itakuwa ni kichocheo cha mabadiliko Afrika nzima
“Kuwepo kwa huduma ya kadi ya Airtel Money Global Pay nchini watanzania watapata Uhuru wa kufanya miamala Kidigitali bila kwenda benki kwa kulipa huduma zote,” amesema Kasegenya na kuongeza kuwa huduma hii imewezekana nchini kwa ushirikiano baina ya Airtel Money Tanzania na Mastercard kupitia Teknolojia ya Mtandao wa Kimataifa
Ameongeza kuwa huduma hii itawafaa sana wafanyabiashara na wanafunzi kwa kuwawezesha kufanya malipo mahali popote na muda wote kwa usalama na uhakika
Kasegenya amesema Artel Money Global Pay ni uvumbuzi wa kipekee unaodhihirisha dhamira ya Airtel katika kuendeleza urahisi wa kidijitali, usalama wa miamala na ujumuishaji wa kifedha kwa wote.
“Ushirikiano huu wa kuunganisha mtandao wa malipo wa Mastercard ndani ya mfumo wa Airtel Money ni hatua kubwa katika kuimarisha miundombinu ya kifedha ya kidijitali hapa nchini.” amesema Kasegenya
Amesisitiza kuwa Airtel Money Global Pay inaendana moja kwa moja na vipaumbele vya Benki Kuu ya Tanzania kuhusu mifumo ya malipo, ujumuishaji wa kifedha, na kuondoa mipaka ya matumizi ya fedha. na pia hduma hii ni njia salama na rahisi kwa watanzania wenye akaunti za benki na wasio nazo kushiriki katika uchumi wa kidijitali wa dunia
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba, ameeleza kuhusu umuhimu wa Airtel Money Global Pay kwa kusema itawezesha kupanua wigo wa huduma za malipo ya kimataifa kwa wateja wa Airtel Tanzania.
“Tumewarahisishia wateja wetu kufanya malipo ya kimataifa kutoka hapa nchini bila kuhitaji akaunti ya benki. Pakua tu MyAirtel App, wasilisha maombi ya Global Pay, weka salio na anza kufanya manunuzi, kuangalia filamu au kulipia huduma zako kimataifa kwa urahisi na usalama,” amesema Rugamba