Na Lilian Ekonga....
Waziri wa Nchi, ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Mhe Geogre Simbachawene ametoa amewataka wahitimu wa Taasisi ya Uongozi Institute kutafuta namna bora zaidi za kuratibu utekelezaji wa miradi katika njia itakayosaidia matumizi ya rasilimali fedha na watu ili kuleta matokeo makubwa na chanya.
Rai hiyo ameitoa leo Mei 16 katika Mahafali ya Nane(8) ya Programu za Uongozi zinazotolewa na Taasisi ya Uongozi yaliofanyika jijini Dar es salaam
Amesema Serikali imewekeza pesa nyingi sana katika miradi hiyo ili kuleta maendeleo na kuimarisha ustawi wa wananchi jambo ambalo litaimarisha mawasiliano na mahusiani na wadau wetu wa maendeleo ndanu na nje ya mipaka ya nchi yetu.
"Mmefundishwa masuala muhimu ya maadili na utawala bora pamoja na athari za rushwa katika kutekeleza majukumu yeny kama watumishi, yote haya yatoshe kusema sasa tunataka kuona utumishi bora wenye misinhi imara na tahabiti ya kiongozi na hatutegemea kuona mnaowaongoza au nyie wenyewa mkijihusisha na maswala ya Rushwa" amesema Simbachawene
Ameongeza kuwa Dhima Kuu ya mahafali Hayo ni kukuza uongozi wa Mabadiliko kwa maendeleo Endelevu Barani Afrika na Agenda ua Umoja wa Afrika 2063 inayonyesha viongozi wana changamoto kubwa ya kujenga Bara la Afrika lenye taswira bora zaidi.
Aidha Waziri Simbachawene,amesisitiza umuhimu wa kufanyia marekebisho mchakato wa kuwathibitisha Wakurugenzi Wakuu ili kuepusha migogoro
Awali akizungumza Mke wa Rais wa Finland, Suzanne Innes-Stubb, amewashauri viongozi nchini kukumbatia maadili, uadilifu, utawala bora na kufanya maamuzi kwa kuzingatia ukweli.
Pia alitoa tahadhari kwa madhara ya taarifa potofu na upotoshaji ni makubwa, hivyo viongozi wanapaswa kufanya maamuzi kwa kuzingatia ukweli na si kwa dhana au hisia.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said, aliwahimiza viongozi kutumia ujuzi walioupata kuwahamasisha wengine na kuchangia maendeleo yenye maana.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uongozi, Kadari Singo, amesema tukio hilo limeandaliwa kusherehekea mafanikio ya waliokamilisha programu za muda mrefu za taasisi hiyo: Stashahada ya Uzamili ya Uongozi (PGD), Cheti cha Uongozi (CiL), na Mpango wa Uongozi wa Wanawake (WLP).
Ameongeza kuwa zaidi ya viongozi 200 wamehitimu katika programu hizo tatu, ambazo zimehudhuriwa na viongozi kutoka bara zima – na kutoka sekta mbalimbali kama serikali, biashara, elimu ya juu na asasi za kiraia.
Singo amesema programu hizo tatu zinalenga kukuza ujuzi wa uongozi katika maeneo ya uongozi binafsi, uongozi kwa watu, na uongozi wa taasisi.