TAMASHA LA MTOKO WA PASAKA KUKUTANISHA WAIMBAJI WA INJILI KUTOKA NDANI NA NJE YA TANZANIA







Na mwandishi wetu.....

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steve Mengele maarufu kama "Steve Nyerere" amesema kuwa siku ya sikuu ya Pasaka litafanyika tamasha kubwa la "mtoko wa Pasaka" ikiwa ni sehemu ya kuwakutanisha pamoja Watanzania na kufurahia kupitia nyimbo za injili.

Taarifa hiyo ameitoa leo April,8,2025 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari huku akisema kuwa tamasha hilo litakua la aina yake kwani linashirikisha waimbaji kutoka ndani na nje ya Tanzania.

"Maombi yana nguvu kuliko mtutu wa bunduki,maombi yana nguvu kuliko matusi,maombi yana  nguvu kuliko kitu kingine chochote,hivyo siku hiyo tutaliombea Taifa na Rais Wetu Mpendwa Dkt Samia Suluhu Hassan"amesema

Nakuongeza kuwa "sisi tumeona ndani ya mwezi huu(April)kulikua na mambo mengi ikiwemo ramadhani, kwaresma,na sasa tunelekea kwenye sikukuu ya Pasaka,hivyo kuelekea kilele cha sikukuu ya pasaka tutatoa pakeji ya vifaa vya kumsaidia mama mjamzito kujifungua katika Hospitali zote za Wilaya Mkoani Dar es salaam" 

Steve Nyerere amempongeza muimbaji  mkongwe wa nyimbo za injili Christina Shushu kwa kuandaa tamasha la mtoko wa pasaka litakalofanyika siku ya pasaka April,20,2025 katika ukumbi wa Superdome Masaki kuanzia saa saba mchana.

"Watakuwepo waimbaji wote nguli wa nyimbo za injili kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania Kenya,Uganda na kwingineko,ambapo  watashiriki katika tamasha hilo ambalo halitakua na kiingilio lenye kauli mbiu isemayo "Kwa maombi utashinda"

                       
Kwa upande wake Mwimbaji wa Nyimbo za injili Christina Shushu,amesema kwamba tamasha la "mtoko wa pasaka"  ni kuwaleta Watanzania pamoja na raia wa mataifa mengine ili kufurahi kwa pamoja kupitia nyimbo na muziki wa injili. 

"Waimbaji wengi watakutana na kufurahi lakini kwasababu ni Mwaka wa uchaguzi tutamuombea Mama yetu Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi anazozifanya za kuliongoza Taifa la Tanzania".amesema Christina Shushu

Amesema kuwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao imekua ikifanya mambo mengi ya kijamii,hivyo yeye kama mwanachama wa Taasisi hiyo ameamua kuandaa tamasha la nyimbo za injili siku ya sikukuu ya pasaka April 20,2025 ili kufurahi pamoja na jamii.

"Tumealika na watu wa nje ili waje waone siri ya amani ya nchi ya Tanzania,manake wengi wanajua Tanzania ni nchi ya amani lakini siri ya amani uliyopo hawaijui". amesema




Previous Post Next Post