RC CHALAMILA MSINGI WA MALEZI BORA NA MAKUZI YA MTOTO NI MUHIMU KWA MASILAHI MAPANA YA TAIFA




-Amshukuru Rais Dkt Samia  kwa kuwa kinara katika kuhakikisha watoto wanapatata misingi bora ya makuzi, malezi na maendeleo yao.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo mapema leo Machi 12,2025 wakati akifungua kikao cha Tathimini ya utekelezaji  wa programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto-PJT MMMAM ( Naional Mult-sectoral Early  Childhood Development Program) kwa kipindi cha Oktoba- Desemba 2024.

RC Chalamila amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa katika kuhakikisha  kuwa watoto wanapata msingi bora wa  Makuzi, Malezi, na maendeleo yao.

Aidha RC Chalamila amesema kikao hiki cha tathimini ya utekelezaji wa PJT-MMMAM ni fursa adhimu ya kutafakari maendeleo yaliyopatikana katika kipindi  cha mienzi mitatu iliyopita, kujadili changamoto na kupanga mikakati ya kuboresha  utekelezaji wa Programu kwa kipindi kinachofuata

Kwa upande wa Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila akimkaribisha Mkuu wa Mkoa amesema Programu hiyo ilizinduliwa Dec 13, 2021 ikiwa na lengo la kuhakikisha watoto wanakua na kufikia kiwango cha juu kabisa cha  Maelezi, Makuzi  na Maendeleo yao ya awali ambapo amesema Mkoa unaendelea kufanya vizuri katika masuala ya lishe bora ambapo hadi sasa Mkoa uko katika kiwango cha chini kabisa cha udumavu hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuondoa kabisa changamoto hiyo.




Vilevile Dkt Toba Nguvila amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa wabunifu, na kutumia mbinu mbalimbali zenye kulenga kuifikia jamii kwa ukubwa wake. 

Hata hivyo RC Chalamila amesistiza lazima tuhakikishe kila mtoto anapata hiduma bora za Malezi, Makuzi, na Maendeleo ya Awali ili aweze kufikia kilele cha maendeleo yake Kimwili, Kihisia, Kiroho na kijamii hii inawezekana kwa kuimarisha ushirikiano wetu, kuishirikisha jamii ipasavyo  na kuhakikisha rasilimali za kutekeleza programu hii zinapatikana.

Mwisho kikao hicho muhimu kimehudhuriwa na  Mganga Mkuu wa Mkoa, mratibu wa programu jumuishi, viongozi wa Dini, waratibu na wataalamu wa programu hii ngazi za Halmashauri, Watalaam kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na wadau wengine wa utekelezaji wa programu ya MMAM kutoka katika mashirika ya kimataifa, Kitaifa na Asasi za Kiraia.





Previous Post Next Post