Na Lilian Ekonga......
Waziri wa elimu sayansi na Teknolojia prof Adolf mkenda amekitaka chuo cha ufundi na mafunzo stadi nchini VETA kujenga tabia ya kushirikina na kampuni zilizopo katika soko ili kufahamu uhitaji wa soko pamoja na ujuzi ili kuboresha eneo la ufundi stadi ambalo limekuwa mkombozi wa ajira nchini
Prof Mkenda ameyasema hayo wakati akizungumza na wadau wa sekta ya nguo na mavazi wakati wa kongamano lililokutanisha wadau wa sekta ya nguo na mavazi ikiwa ni maadhimisho ya miaka 30 ya chuo cha veta ambapo amesema ili kufikia malengo ya kujenga vijana watakao endana na soko ni lazima veta ikijenga mahusiano na ushirikiano na kampuni za uzalishaji ili kubaininsoko linataka nini
"Tunahutaji sana kufanya kazi na nyie kuimarisha ujuzi tunao utoa katika vyuo vyetu vya veta vitu sio vya nadharia na wanafunzi wanahitaji kujifunza zaidi kwa vitendo na tunawahitaji nyie katika hilo" amesema Mkenda.
Aidha amekipongeza chuo cha Ufundi stadi Veta kwa kutekeleza maagizo ambayo amekuwa akitoa kuhusiana na kuboresha baadhi ya maeneo na kuboresha eneo la ufundi stadi eneo ambalo limekuwa mkombozi wa ajira nchini
Kwa upande wake Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia Elimu Dkt, Charles Wilson Mahera amesema mkutano huo utasaidia kuwapanujuzi wadau hao ili kuendana na mahitaji ya viwanda na hivyo kuongeza thamani ya mazao ikiwemo pamba na ngozi
Awali Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Antony Kasore amesisitiza kuwa sekta hiyo imeajiri watanzania wengi hivyo veta itaendelea kutimiza wajibu wake wa kutoa ujuzi unaotakiwa kwa wananchi wengi zaidi ili kutanua wigo wa ajira nchini
.