Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Kichina ya CRJE (East Africa) Limited imesema mradi wa ujenzi ambao upo kwenye hatua za mwisho kabisa wenye thamani ya Tsh10.8 bilioni katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) unatarajiwa kukabidhiwa rasmi kwa Taasisi hiyo iliyo chini ya Wizara ya Uchukuzi mwezi huu.
Kampuni ya CRJE (East Africa) Limited imejenga majengo mawili katika Chuo hicho kupitia Mradi wa Eastern Africa Skills for Transformation and Regional Integration (EASTRIP) ambao umefadhiliwa na Benki ya Dunia wenye lengo la kuendeleza Kituo cha Umaahili katika Usafiri wa Anga.
Akizungumza katika mahojiano jana jijini Dar es Salaam, Dai Yanwei, Msimamizi wa mradi huo kutoka CRJE (East Africa) Limited alisema: “Tumefanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha mradi huu unakamilika mapema iwezekanavyo. Tuna Mshukuru Mungu tumekamilisha salama na hivi sasa tupo kwenye hatua ndogo ndogo za mwisho ili tuweze kukabidhi mradi huu kwa Chuo.”
Mnamo Novemba 2022, NIT imeingia mkataba wa mwaka mmoja na Kampuni ya CRJE (East Africa) Ltd kujenga majengo mawili katika kampasi kuu ya Taasisi hiyo, Mabibo jijini Dar es Salaam.
"Tulitarajiwa kumaliza mradi huu mwaka mmoja baada ya kusainiwa lakini tulikumbana na changamoto baada ya kuanza. Mvua kubwa iliyonyesha mnamo 2023 ilisababisha kuchelewesha kumalizika kwa mradi huu,” Bw Yanwei alisema.
Hata hivyo, CRJE (East Africa) Ltd. ina historia ya kufanya kazi nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka 50. Ilianzishwa mwaka 1969 ili kutekeleza ujenzi wa Reli Kuu ya Uhuru-TAZARA, mradi mkubwa zaidi kuwahi kukamilika nchini kwa ruzuku ya serikali ya China.
Katika viwango vya kimataifa CRJE ni mkandarasi mwenye ubora wa nyota tano.
CRJE (East Africa) Ltd ina wafanyakazi zaidi ya wafanyakazi 5,000 katika nchi za Afrika Mashariki.
Kampuni ya CRJE imeshajenga jumla ya mita za mraba milioni 3 za ujenzi nchini Tanzania ndani ya miaka 50, ikijumuisha zaidi ya miradi 30 ya kihistoria kama vile Daraja la Nyerere, Chumba Kipya cha Mijadala ya Bunge Dodoma, Kituo cha Mikutano cha Dodoma, Chuo Kikuu cha Dodoma, jengo la Rita, Uhuru Heights na Nyerere Foundation Square nk.
Kampuni ya CRJE ndiyo yenye rekodi ya kasi zaidi kwa ujenzi Afrika Mashariki ambapo ina rekodi kwa ya kumaliza sakafu moja ya kawaida ndani ya siku sita. Rekodi nyingine ya kampuni ni kukamilika kwa usanifu na ujenzi wa Kituo cha Mikutano cha Dodoma ndani ya miezi 7, na kutengeneza kasi maarufu ya “Dodoma Speed” nchini Tanzania.
Kampuni pia imejenga hoteli nyingi za kiwango cha kimataifa za nyota tano nchini Tanzania zikiwemo hoteli ya Serengeti Four Seasons na hoteli ya Zanzibar Park Hyatt.
Daraja la Mwalimu Nyerere na miradi mingine mingi mikubwa imekuwa alama nzuri zaidi ya biashara ya kampuni hiyo. Kwa mtindo ubora wa kazi, sifa nzuri na miradi ya hali ya juu, ambapo kampuni imetunukiwa mara tatu ya "Mkandarasi Bora wa Kigeni" nchini Tanzania, na mara mbili "Tuzo ya Luban" tuzo ya Oscar ya China kwa ubora katika ujenzi.
Mwisho