PDT FOUNDATION KUSAIDIA WANAFUNZI WANAOTEMBEA UMBALI MREFU KWENDA SHULENI









Na Lilian Ekonga....


Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya PDT Foundation imepokea msaada wa baiskeli 30 kati ya 150 kutoka kwenye tasisi ya Kwa AMO Foundation zenye  lengo la kuwasidia wanafunzi waanaotembea umbali mrefu zaidi kutoka majumbani kwenda shuleni.

Akizungumza na waandishi wa habari 23,Machi 2025 katika iftari iliyombana na hafla ya kuchangia wanafunzi wa sekondari ya Mubela iliyoandaliwa na  PDT Foundation, Mkurugenzi wa AMO Foundation Amina Said amesema wamechangia baiskeli 30 ikiwa lengo ni kupata baiskeli 150.

"Amo Foundation imechangia baiskeli 30 ikiwa lengo lilikuwa ni baiskeli 150 ambapo tukahakikisha baiskeli 150 zinapatikana zote na wanafunzi wanaotembea umbali mrefu waweze kuhudhuria masomo ipasavyo"amesema

Said Amesema Taasisi hiyo siyo ya kiserikali ila inasapoti kazi za serikali Kwa sababu serikali inawasapoti Taasisi hizo zisizo za kiserikali"serikali haiwezi kuwafikia watu wote mpka chini kabisa ndomana sisi tupo Kwa ajili ya kuiwakilisha serikali pia"Amesema Said

Amesema AMO Foundation inamsaidia mama inamsaidia vijana na watu wenye uhitaji maalumu na inatoa huduma Kwa jamii Kwa kufanikisha Kwa kuungana na watu Wetu wa karibu tutafanikisha kuzipata hizo baiskeli Zaidi ya 150

Aidha amesema wamezungumza na mwalimu kuu wa shule iliyoko muleba amesema Kwa wiki mtoto anaenda mara 3 au mara 2 kutokana na umbali anapotoka mpaka kufika shuleni anatumia kilomita 40 Mpaka Kilomita 20 inafika Muda mtoto anatako asubuhi kujiandaa mpaka afike shuleni anakuwa anaishia njiani na Muda umeisha pia wanakutana na mitihani migumu wakiwa wanaelekea shule.

"Kama Sasa hivi dunia ilivyobadilika unakutana na mtu anakunyanyasa kijinsia watoto wakike wanabakwa tunawaomba taasisi zingine tuguswe Kwa hili Kwa watoto Wetu walioko nje ya mji tuweze kuwasapoti Kwa kufika shuleni Kwa wakati" Ameongeza Said

Nae Mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali PDT Foundation Joyce Charles Amesema wameanza na watoto wa shule ya sekondari kiteme iliyo muleba ambao wanatembea umbali mrefu sana kufika shule kwa kuwasidia baiskeli 150 zitakazowezesha kufika kwa urahisi zaidi.

"Tumegundua tatizo hilo tulipo kuwa safari mimi na rafiki yangu tukaona umbali mrefu wanaotembe kutoka nyumbani kwenda shule ni kama kilomita 20 ambapo kuna misitu na mapori tukawaza tufanye kitu kwa watoto hap kwa kuchangisha baiskeli na kuwawezesha watoto kufika shuleni"amesema charlse






Ameongeza kuwa wamejipanga Kwa mwaka wana tunaprojet nne itakayofata Sasa hivi itakuwa ni mwezi wa sita ni Kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali Kwa kupata ujuzi na vifaa keamtoto aliemaliza fomu 4 anataka kujifunza kushona tutamuita mjasiriamali anaejua.cherehani aje Kwa ajili ya kumfundisha na tutamuezesha kupata cherehani Ili tuweze kuigusa jamii nzima
Mkurugenzi wa ni Adeline Mmary kampuni ni Wiserpal consultancy

Halikadhalika nae Mkurugenzi wa kampuni Wiserpal Consultancy  ,Adeline Mmary Amesema ameguswa sana na project ambayo amekuja nayo PDT kuwasaidia watoto wenye uwitaji Katika vijiji ambavyo usafiri ni changamoto na tumeguswa na kusema sisi tutaenda na kusukuma Ili project iwafikie walengwa na watoto waweze kupata msaada

"Kwa asilimia kubwa tunawaomba watanzania wengine tunaomba kuwasaidia Hawa watoto waweze kupata usafiri kwani wanapata tabu sana"Amesema Mali





Previous Post Next Post