WAKATI Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Dkt Samia Suluhu Hassan akitimiza miaka minne madarakani uongozi wake ,Falsafa yake ya 4R imetajwa kuwa mkombozi kwa watanzania.
Falsafa ya 4R ni Reconcilition(Maridhiano),Resilience (Ustahimilivu),Reform(Mageuzi)na Rebuilding(Kujenga Upya).
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Jijini Dar es Salaam Mwandishi wa Kitabu cha Samia na Falsafa ya SamiaLojia,Derek Murusuri,amesema anaiona falsafa ya Rais kama muarubaini wa utulivu zaidi wa Tanzania na amani ya Afrika na Dunia.
"Katika Bara lililojaa migogoro na vita anuai,Raslimali nyingi za mataifa ya Afrika zinatumika kustawisha migogoro badala ya mazao ya kiuchumi na kushindwa kuwahudimia wananchi wake ipasavyo,ni wakati wa mataifa haya kutumia falsafa ya 4R ni suluhisho"Amesema Murusuri.
Hata hivyo, Murusuri,amekizungumzia kitabu chake cha Samia na Falsafa ya Samialojia,amesema kinatarajia kuzinduliwa tarehe 19 mwezi huu wa tatu ni siku mbayo Rais Samia alipoapishwa na kuanza mageuzi makubwa ya kisiasa,kijamii na kiuchumi.
Amesema Kitabu hiki ni zawadi kutoka kwa wananchi wa kawaida waliona,kuguswa na Utendaji wa Rais katika kuliongoza Taifa na kuwathamini watu wakiguswa na Utendaji wake na kuamua kutunga kitabu.
"Si kumpa moyo Rais Samia ,bali pia kwa kuhifadhi historia ya mambo mazuri yasije yakachukuliwa na upepo"Amesema Murusuri.
Hata hivyo,Mwandishi huyo amesema kitabu hicho kimeandika mambo mengi katika dhana ya uongozi,nguvu ya kiongozi mwanamke na mafanikio yake yanaweza kuigwa na mataifa mengi.
"Hiki ni kitabu cha uongozi unaobadilisha,uongozi wa utumishi.Uongozi unaochochewa na malengo ya kuleta mabadiliko.Si kitabu cha kuweka Kabatini.Ni mwongozi wako katika utumishi wa wanadamu haga Duniani ili kuratibu urathi wako kila utakapokanyaga"