Na liliana Ekonga........
Waziri wa Elimu, Sayansi ya Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Ameipongeza Bodi ya Tume ya Nguvu ya Atom TAEC kwa kutenga bajeti iliyoelekezwa na serikali kwaajili ya kwenda kuwafundisha watanzania nje ya nchi kwenye vyuo bora.
Waziri ameyasema hayo leo Februari 19 jijini Dar es salaam wakati akizundua Bodi ya Tume ya Nguvu ya Atom ambapo amesema serikali imetenga fedha kwa ajili ya Mafunzo ya Muda mrefu ya vyuo vikuu nje ya nchi.
"Kipaumbele cha kwanza ni kwa watumishi wa tume na wapili ni katika vyuo vikuu kwa wale amabo watakidhi vigezo, tunajua tukiwaendeleza tutakuja kuwa na watu wazuri, amesema Prof. Mkenda
Ameongeza kuwa Samia Scholarship Extended Kwa ajili ya kuwapeleka watanzania kwenda kusoma kwenye vyuo Bora kabisa hapa dunia kwenye mambo ya Atom,Nyuklia Kwa ajili ya kuendeleza fani hapa nchini
"Tanzania Katika eneo hili lipo vizuri sana kuliko nchi nyingine na wageni wanakuja hapa,lakini tunasema Bado tunauhitaji wa kwenda umbali zaidi,sisi tunamadini ya Uraniam lakini Kuna probability nyingi tu lakini hatujazi kutumia vizuri,maswala ya tiba Kwa kutumia nishati ya Atom (Miyozi),na halikadhalika na mambo ya kilimo,Tunaitaji kuwa na nguvu kubwa"Amesema Mkenda
Pia Waziri Mkenda Amesema swala la scholarship ya kwenda nje mara nyingi ni la serikali japo nchi nyingi zipo tayali kukupa msaada ila kutoa scholarship sio common sana.
Mkenda ametoa angalizo Kwa Tume."Twendeni tukajifunze Katika vile vyuo Bora ambavyo mulivyonionesha wenyewe tukawapeleke watanzania wakasome Kwa Bajeti hiyo na mliyoitenga,Kwa hili Bodi ningependa liendelee na mlisimamie"Amesisitiza Mkenda
"Na tunawapa final disisheni na hamna haja ya kuja wizarani nyie sio Idara ya wizara ya elimu sayansi na teknolojia nyie ni taasisi ambayo inayofanya kazi, Bodi hiyo inayofanya kazi Kwa niaba yetu sisi,tunawapeni mamlaka ya kuchagua na kuwapeleka kulingana na sisi miongozo tuliyoitoa"
Aidha Amesema tunawapa kipaumbele Tume yetu ya ndani Kwa usajili huo wa mastazi au Phd kwani hatuwezi kuwaacha watu Wetu wa ndani,pia Kwa vyuo vikuu Kwa wale wanaouhitaji Kwa kuwaendeleza Kwa kuwatumia vizuri kwani Bajeti ipo watanzania wakasome
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TAEC Joseph Msambichaka amemshukuru RAIS samia Kwa kuweza kumchagua Katika Tume hiyo ya ukurugenzi wa Bodi ya TAEC kwa kipindi cha pili kuanzia june 2024
Nae Mkurugenzi Mkuu wa TAEC Prof.Najat Mohammed amesema TAEC watendelea na majukumu yap ya kudhibiti na kuhamasisha matumizi ya teknlojia mpya nchini kwa mujibu wa sheria huku akisitiza kuwa wamewapokea wajumbe wote walioteuliwa.