KIVUKO MV. KILINDONI CHASIMAMA KUTOA HUDUMA MAFIA





Kivuko MV. KILINDONI kinachotoa huduma kati ya Mafia Wilayani Mafia na Nyamisati Wilayani Kibiti Mkoani Pwani kitasimama kutoa huduma katika eneo hilo kuanzia siku ya leo Tarehe 12 Februari, 2025 ili kupisha matengenezo pamoja na kufungwa injini mpya.


Kivuko MV. KILINDONI kimewasili leo kikiwa na abiria pamoja na mizigo eneo la Nyamisati kikitokea Wilayani Mafia.


Kivuko hicho kinatarajiwa kupekekwa Mkoani Dar es Salaam ambako kitakuwa huko kwa muda wa wiki moja kikifanyiwa matengenezo hayo ili kukiongezea ufanisi kiweze kurejea kikiwa bora na salama kwa watumiaji.


Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), unawaomba radhi abiria wote kutokana na usumbufu watakaoupata kutokana na kukosekana kwa huduma ya kivuko hicho.



Previous Post Next Post