Na Lilian Ekonga.......
SHIRIKA la Foundation For Civil Society (FCS) limeingia makubaliano ya miaka miwili na Benki ya Stanbic Tanzania kupitia mradi wa Stanbic Biashara Incubator unaolenga kuwainua wajasiriamali wanawake na vijana kwa kuwapatia ujuzi, maarifa, na fursa za ukuaji wa biashara maeneo ya mipakani.
Akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano hayo jijini Dar es Salaam leo februari 20 , MKurugenzi wa FSC, Justine Rutenge amesema makubaliano hayo baina ya fsc na stanic biashara Incubator ya lengo ya kuwakwamua kiuchumi wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu katika kujipatia ajira na kujiinua kiuchumi kwa kuwawezesha kutumia vizuri fursa za masoko ndani na nje
"Tunajikita katika kuhakikisha sauti za wananchi zinasikika na kwa kushirikiana na sekta za umma na binafsi, tukiwezesha wafanyabisahara kupata masoko" amesema Rutenge
Ameongeza kuwa miradi ipo miwili na mradi wa kwanza utaangazia wajasirimali na wasidikaji wa mazoo ya mbogamboga, matunda pamoja na mwani katika kuhakikisba wanaongeza dhamani ya mazao yao na walengwa ni wafanyabishara walioko Dar es salaa na mradi wa mwingine utaangazia wanawake wanaofanya biashara za mipakani.
Aidha amesema mradi unafadhiliwa na TradeMark Afrika (TMA) kwa msaada wa serikali za uingereza kupitia FCDO, Ireland na Norway.
"Tunafurahi ubia wetu wa kihostoria na stanbic bank kupitia mradi wao stanibic Biashara Incubator ambao utasaidia kuvuna ujuzi wa wenzetu katika kuwafikaia wananchi kwa ufanisi zaidi"amesema Rutenge.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Stanbic Biashara Incubator, Kai Mollel amesema kuwa lengo ni kuwawezesha wajasiriamali ili biashara zao ziweze kustawi na kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye uchumi wa taifa.
“Tunatambua kuwa biashara ndogo na za kati (SMEs) ndizo zinazotoa mchango mkubwa katika ujenzi wa uchumi wa Tanzania. Zinatoa ajira kwa mamilioni ya watu na zina mchango mkubwa katika pato la taifa,”
“Hata hivyo, changamoto bado ni nyingi katika sekta hii, ikiwemo ukosefu wa elimu ya kifedha na mbinu bora za kusimamia biashara, changamoto za mitaji, na upatikanaji wa masoko,” amesema Mollel.
Ameongeza kuwa kwa wafanyabiashara wa mipakani, changamoto ni kubwa zaidi kutokana na vikwazo vya kisheria, ukosefu wa taarifa sahihi, na mazingira magumu ya kufanyia biashara, hali inayowafanya washindwe kufanikisha shughuli zao kwa urahisi na ufanisi.
“Benki ya Stanbic Tanzania inaamini kuwa Tanzania ni nyumbani kwetu, na hatuwezi kuwa na uchumi imara bila kuhakikisha biashara ndogo na za kati zinapata uwezeshaji wa kweli. Kupitia Biashara Incubator, tunajitolea kuwawezesha wajasiriamali kukuza biashara zao kwa viwango vya juu zaidi,” ameongeza Mollel.
Katika ushirikiano huu, wajasiriamali 250 wa mipakani na 100 wa Programu ya Ukuzaji wa Wasambazaji watapokea mafunzo maalum. Mafunzo haya yanajumuisha siku nane za stadi za uzabuni na mafunzo ya biashara yanayotolewa na Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) ili kuwaandaa kushiriki kikamilifu kwenye minyororo ya thamani ya makampuni.
Nae Meneja Mradi wa Fsc Chaelse Kainkwa amesema Mradi huo utajumuisha wajasirimali w mbogamboga, matunda na Mwani ambao watapatiwa mafunzo mbalimbali yanayohusu mambo ya ukuaji wa biashara na upatikanaji wa fedha kama mikopo.
"Kwenye upande wa Fcs tutawaleta wadau wengine ambao watakuja kutoa mafunzo mbalimbali ikiwemo jinsi ya kuongeza dhamani ya mazao yao pia wataunganishwa na wadau mbalimbali kama Brela, TBS na Wadau wengine" amesema